2014-11-15 12:01:55

Papa Francisko kuunguruma FAO hapo tarehe 20 Novemba 2014


Shirika la kilimo na chakula la Umoja wa Mataifa FAO; kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani, WHO, kuanzia tarehe 19 hadi tarehe 21 Novemba 2014 watafanya mkutano wa kimataifa, utakaowashirikisha mawaziri wa afya na kilimo wapatao 100; Wawakilishi kutoka katika nchi 190 pamoja na viongozi mashuhuri, ili kuzungumzia mikakati ya kukabiliana na baa la njaa, utapiamlo wa kutisha miongoni mwa Watu wa Mataifa.

Baba Mtakatifu Francisko ni kati ya viongozi mashuhuri watakaotoa hotuba katika mkutano wa pili wa lishe utakaofanyika kwenye Makao makuu ya FAO, mjini Roma. Ratiba inaonesha kwamba, Baba Mtakatifu atahutubia mkutano huu hapo tarehe 20 Novemba 2014. Mkutano huu utafunguliwa rasmi tarehe 19 Novemba kwa ujumbe kutoka kwa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki-Moon. Viongozi kutoka FAO, WHO watatoa pia hotuba katika siku ya kwanza ya mkutano.







All the contents on this site are copyrighted ©.