2014-11-15 07:42:08

CD ya "Habemus Papam" imeanza kupasua mawimbi!


Baba Mtakatifu Francisko, hivi karibuni alipata fursa ya kusikiliza nyimbo mbali mbali zilizoimbwa wakati wa mkutano wa Makardinali walipokuwa wanajiandaa kwa ajili ya uchaguzi hadi siku ile Baba Mtakatifu Francisko alipoanza utume wake rasmi, kama Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Hizi ni nyimbo zilizokusanywa katika CD mbili na zimeimbwa na Kwaya ya Kikanisa cha Sistine. Kwa sasa CD hizi inauzwa kwenye maduka mbali mbali nchini Italia na baada ya muda si mrefu CD hizi zitaweza kupatikana kwa watu wengi zaidi. CD hizi zimetengenezwa kwa ushirikiano kati ya Kampuni ya Deutsche Grammophon kutoka Ujerumani kwa kushirikiana na Radio Vatican.

Uzinduzi wa CD hizi ulihudhuriwa na viongozi kadhaa kutoka Vatican akiwemo Monsinyo Massimo Palombella, Mkurugenzi wa Kwaya ya Sistine, Padre Federico Lombardi, Msemaji mkuu wa Vatican na Mkurugenzi wa Radio Vatican pamoja na viongozi na wafanyakazi kutoka Kampuni ya Deutsche Grammophon ya Ujerumani. CD hii inakwenda kwa jina la "Habemus Papam" yaani "Tumepata Papa".







All the contents on this site are copyrighted ©.