2014-11-14 15:22:51

Kuweni mfano wa Imani kimatendo si kwa maneno... Papa


Kufundisha imani kwa watoto na vijana leo hii, ukweli na upendo,v inapaswa kuwa utendaji wa maisha ya kila siku ya watu wazima, katika kuwa mfano wa jinsi ya kuishi,kuwa mfano halisi na si kwa maneno mengi. Papa Francis alieleza leo hii , katika hotuba yake wakati wa Misa, katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta , Ibada iliyohudhuriwa na kundi kubwa la watoto na vijana, waliomtembelea mapema Ijumaa hii kutoka Parokia za Roma.

Papa alilenga katika jinsi ya kuieneza imani katika ulimwengu wa leo wa vifaa vya digital, akisema, njia inayofaa zaidi ni kuwa na maisha yanayoleta msisimko katika imani. Ni kwa mfano wa maisha yanaongoza vijana katika kuona ahadi na matumaini ya ulimwengu ujao.

Papa aliendelea kutazama masomo ya siku, akisema yanahimiza kutembea katika upendo na ukweli. Si kufundisha kwa maneno, lakini kupitia utendaji wa kila siku kimaisha mzazi anaweza kuirthisha imani yake kwa watoto wake. Na ni wajibu wa kwanza kwa Mkristo kuieneza imani yake kwa watoto wake. Mkristo anawajibika kuwatunza watoto na kuirithisha imani yake, katika kile anachokiamini ndani ya moyo wake, hata kwa watoto wake.

Kila kitu, anasema Papa Francisco, hutegemea sana mtazamo sahihi unaoelekezwa kwa watoto. Na ni - swali ambalo bado linamgeukia mzazi na mtazamo wa ndugu, baba, mama, dada, kaka , katika majiundo na tabia ya makuzi, kukua kama kikosi, au kila mtu na maisha yake.

Kwa maana hiyo, jamii yote inatakiwa kuona wajibu wa kutenda vyema, na kuonyesha imani sahihi kwa machipukizi ya jamii. Vijana hawana haja ya maneno mengi, bali vitendo. Leo hii maneno si muhimu! Katika dunia hii ya digital, ambamo kila mmoja ana simu, maneno hayatumiki tena. Lakini kinachohitajika ni vitendo, kuwa mfano katika mienendo ya maisha.
Papa Francisco alieleza na kuwarejea vijana wanaopokea kwa mara ya kwanza sakramenti ya communio, au wale wanaopata sakramenti ya kipaimara, jinsi wanavyo paswa kuzingatia kimatendo maangano na kuufungua mlango kwa maisha ya Kikristo" mara baada ya kuanza njia ya maisha kuelekea hatima yake kama ilivyoelezwa katika Barua ya Yohana kwa watu wote. Ni kutembea katika ukweli na upendo, hadi kufikia sakramenti nyingine kama vile ndoa. Lakini njia hii, inahitaji kijana kujua namna ya kuishi, kujua jinsi ya kuishi kama Yesu.

"Papa alitoa ufafanuzi juu ya Sakramenti, huku akisisitiza muumini kupata muda wa kukutana na Mungu kupitia ibada za sala na maombi. Tunahitaji kuomba. Maombi ya pamoja, kumwomba Bwana Yesu kumwomba kwa Mama yetu, asaidie katika safari hii ya ukweli na upendo. Papa aliwahimiza watoto hao kila siku kwenda kukutana na Yesu madhabahuni. Yesu ambaye ni madhabahu yenyewe humtaka kila muumini kutembea katika ukweli na upendo. Papa aliwakaririsha watoto maneno hayo ,kutembea katika ukweli na upendo.








All the contents on this site are copyrighted ©.