2014-11-12 15:26:17

Vatican kuunda bodi mpya kushugulikia makosa ya kinjisia


Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa limechapisha Barua binafsi ya Papa “Motu Proprio’ Sacramentorum Sanctitatis Tutela ’ (SST) ya 30 Aprili 2001, iliyopitishwa pia Mei 21, 2010, yenye maelezo bayana juu ya haki za kisheria za kutoa hukumu kwa makosa, ya unyanyasaji wa kijinsia, chini ya Mamlaka ya Baraza la Kipapa la Mafundisho tanzu ya Kanisa, (Rej. Kipengere namba 1-6), kwa mujibu wa Ibara . 52 ya Katiba ya Kitume ya Kristo Mchungaji mwema.

Katika hukumu ya uhalifu uliotajwa hapo juu , Baraza la Kipapa la Mafundisho tanzu ya Kanisa, linao uwezo wa kuendelea kupitia mchakato wa makosa ya jinai kimahakama au kiutawala kama ilivyo elezwa katika kipengere cha Katiba namba 21 § 1 na § 2, n. 1 SST, chini ya uwezekano wa moja kwa moja kuwasilisha uamuzi wa Mahakama kwa Papa kwa kesi kubwa zaidi ( 21, § 2, n. 2 SST). Na pia katika kutambua uhalifu dhidi ya imani, kwamba mamlaka ina fursa ya kuchukua hatua za kwanza za kawaida katika hirakia ya utawala wa Kanisa( 2 § 2 SST).

Kutokana na wingi wa rufaa na haja ya kuhakikisha uchunguzi zaidi wa haraka unafanyika kwa kesi zilizowasilishwa, baada ya kutafakari kina, Katibu wa Jimbo la Papa, Kardinali Pietro Parolin, tarehe 3 Novemba 2014 aliandika maamuzi ya Papa Francisco juu ya jambo hili kwamba, Baba Mtakatifu Francisko, ameamua kama ifuatavyo:
1.Baraza la Kipapa la Mafundisho tanzu ya imani, litakuwa na bodi maalum , itakayoundwa na Makardinali Saba au Maaskofu wakiwa ni wajumbe wa Shirika kutoka ndani ya Baraza au nje ya Baraza.
2. Rais na wajumbe wa Bodi watateuliwa na Papa. 3. Bodi itakuwa ni sehemu ya vikao vya kawaida (Feria IV) vya Shirika, ambacho kitachambua kwa ufanisi zaidi malalamiko ya kesi , kwa mujibu wa sheria 27 SST, bila ya kubadilisha ufahamu wake wa kitalaam chini ya ibara. 27 SST;
4. Na iwapo mkosaji yuko katika hadhi ya kiaskofu, maombi yake yataamuliwa na Kikao cha kawaida, na kulingana na maoni ya Papa, na pia kesi nyingine zitategemea maoni ya Bodi.
5. Maamuzi ya Bodi, yatatolewa katika taarifa za Shirika za mara kwa mara, baada ya vikao vyake vya kawaida.
6. kwa kanuni maalum ya maamuzi katika taratibu za uendeshaji wa ndani ya Chuo, Baba Mtakatifu Francisko ametoa agizo kwamba, amri hii ni rasmi na ichapishwe katika gazeti la Vatican la L'Osservatore Romano, Novemba 11, 2014, na katika gazeti rasmi la rasmi la Vatican, “Acta Apostolic Sedis”











All the contents on this site are copyrighted ©.