2014-11-12 09:32:49

Siku ya 5 Kimataifa ya kupambana na homa ya mapafu!


Shirika la kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF, katika maadhimisho ya Siku ya Tano ya Kimataifa ya kupambana na Ugonjwa wa Homa ya Mapafu, inayoadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 12 Novemba, linasema kwamba, idadi ya watoto wanaofariki dunia kutokana na ugonjwa wa homa ya mapafu imepungua kwa asilimia 44%, ingawa bado Jumuiya ya Kimataifa inapaswa kujizatiti zaidi, kwani watoto chini ya umri wa miaka mitano wanaendelea kupoteza maisha yao kwa magonjwa yanayoweza kuzuilika!

Mickey Chopra, Mkurugenzi wa afya ya umma UNICEF anasema, hata hivyo hakuna sababu kwa Jumuiya ya Kimataifa kujipongeza kwa hatua hii iliyofikiwa kwani kuna watoto wanaoendelea kuteseka kutokana na umaskini, njaa na utapiamlo. Kumbe, jitihada za kuokoa maisha ya watoto hazina budi kuwafikia watoto wengi zaidi kwa kupambana na magonjwa yanayosababisha vifo vya watoto wadogo, kwa kukazia chanjo, uchunguzi wa magonjwa pamoja na tiba makini.

UNICEF inawataka wafanyakazi katika sekta ya afya kuhakikisha kwamba, wanaendeleza tafiti zinazopania kupambana na hatimaye, kutokomeza ugonjwa wa homa ya mapafu kwa kuhakikisha kwamba, watu wanapata dawa bora kwa bei nafuu.







All the contents on this site are copyrighted ©.