2014-11-12 11:47:07

JK mgonjwa kafanyiwa operesheni Marekani


Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania aliyefanyiwa operesheni ya tezi dume huko Baltimore, Maryland, Marekani mwishoni mwa juma, anaendelea vyema na tayari ameanza kufanya mazoezi kadiri ya taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

Rais Kikwete anawashukuru watanzania na watu wote wenye mapenzi mema wanaoendelea kusali na kumwombea dua jema ili aweze kupona hatimaye, kurudi Tanzania kuendelea na shughuli za ujenzi wa taifa. Taarifa inawaomba wananchi kuendelea kusali kwa ajili ya Rais Jakaya Kikwete.







All the contents on this site are copyrighted ©.