2014-11-12 15:37:57

Barua ya Papa kwa Waziri Mkuu wa Australia, Mkutano wa G20; Maisha hatarini


(Vatican Radio) Papa Francisco ameandika barua kwa Waziri Mkuu wa Australia, Tony Abbot, ikiwa ni kabla ya Mkutano wa maka wa Kikundi cha nchi za G 20, utakao funguliwa rasmi mwishoni mwa wiki hii Brisbane. Katika barua hiyo, Papa anawaomba viongozi wa mkutano huo unaotazama masuala ya uchumi duniani, viongozi kutoka mataifa 20 mashuhuri duniani , kutosahau kwamba maisha ya watu wengi, yanawekwa hatarini, nyuma ya majadiliano haya ya kisiasa na kiufundi.

Papa ameandika, itakuwa kwa hakika ni jambo la kusikitisha kama majadiliano yatabaki katika ngazi za kanuni za maazimio, huku mamilioni ya watu wakiendelea kuteseka na maisha ya wengi kuwekwa hatarini. Papa amebainisha maeneo maalum yanayogusa umma wa dunia kwa wakati huu yanayohitaji utendaji na si maneno, hasa katika kukabiliana na utapiamlo, ukosefu wa ajira (hasa miongoni mwa vijana), ongezeko la kutengwa, na mashambulizi dhidi ya mazingira.


Akizungumzia majibu ya mgogoro wa sasa wa kijeshi, Papa Francisco anasema "dunia nzima" inasubiri uratibu wa makubaliano ya Umoja wa Mataifa, kwa ajili ya kusitisha ubabe wenye ukatili na dhuluma, zinazo elekezwa katika makundi mbalimbali ya kidini na kikabila, ikiwa ni pamoja na watu wachache, katika Mashariki ya Kati" . Anaongeza "Ni imekuwa zaidi na zaidi dhahiri kwamba ufumbuzi wa tatizo hili, haliwezi kupatikana kupitia juhudi za kijeshi, lakini pia ni lazima kuketi pamoja katika majadiliano na wale ambao kwa namna moja au nyingine, wanahimiza vikundi vya kigaidi kupitia msaada wa kisiasa, kinyume cha sheria ya mafuta ya biashara au utoaji silaha na teknolojia. Pia kuna haja kutoa elimu na ufahamu kwamba dini haiwezi kutumiwa kama njia ya kuhalalisha vurugu.


Katika barua hiyo, pia Papa Francisco , ameomba msaada kwa ajili ya waathirika wa migogoro, hasa wakimbizi, akiitazama kwa kina hali katika Mashariki ya Kati, ambayo imefufua mjadala kuhusu wajibu wa jumuiya ya kimataifa katika kulinda watu binafsi dhidi ya mashambulizi yanayo kiuka haki za binadamu na kutokuzingatia kwa sheria ya ubinadamu. Jumuiya ya kimataifa, na hasa nchi wanachama wa G20, lazima pia kutoa tamko lao tahabiti katika haja ya kulinda raia wa nchi zote kutokana aina ya uchokozi mbalimbali unao fanyika kichinichini, madhara yake ni dhahiri tena makubwa. Papa ameeleza akisema, pia anaaminisha hasa ukiukwaji katika mfumo wa fedha, kama ilivyotokea na kusababisha kipeo cha fedha tangu 2008, na kwa ujumla zaidi, ukosefu wa vikwazo vya kisiasa au kisheria katika mawazo ya wachache kutaka kujipatia faida katika shughuli zote za kiuchumi. Ubinafsi huo wa wachache , unakuwa kizingiti kikubwa katika kuwa na amani au haki kwa watu duniani.








All the contents on this site are copyrighted ©.