2014-11-12 09:46:22

Afrika Magharibi yakumbwa na uhaba wa chakula!


Umoja wa Mataifa unaonya kwamba, mlipuko wa ugonjwa wa Ebola ambao kwa sasa ni janga la kimataifa unaendelea kusababisha uhaba mkubwa wa chakula kwa wananchi wanaoishi Afrika Magharibi. Nchi hizi zinaendelea kupambana kufa na kupona na virusi vya Ebola, lakini kwa wakati huo huo zinakabiliana na uhaba mkubwa wa chakula, kwani wakulima wengi wamejikuta wakiacha kushughulikia masuala ya kilimo kwa kuhofia usalama wa maisha yao, hali ambayo imepelekea uwepo wa mfumuko wa bei ya mazao ya chakula.

Sekta ya kilimo ndio uti wa mgongo kwa nchi nyingi za Afrika Magharibi, lakini mfumuko wa ugonjwa wa Ebola umepelekea nchi nyingi kufunga mipaka yake, biashara kuzorota na wawekezaji kutoka ndani na nje ya Afrika Magharibi kusuasua kuwezeka katika maeneo haya, hali ambayo imechangia kupungua kwa uwezo wa wananchi kununua bidhaa na huduma zinazotolewa sokoni. Miundo mbinu mibovu ya barabara na hifadhi ya chakula inakwamisha jitihada za kuwa na uhakika wa usalama wa chakula, changamoto kwa Jumuiya ya Kimataifa kuhakikisha kwamba, inalishughulikia tatizo la uhaba wa chakula Afrika Magharibi, kabla hali haijawa mbaya zaidi!.







All the contents on this site are copyrighted ©.