Zaidi ya wanafunzi 48 wameuwawa kikatili nchini Nigeria
Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu uliopita
alitangaza hali ya hatari kwa majimbo yaliyoko kaskazini mwa Nigeria, ili kupambana
na vitendo vya kigaidi vinavyofanywa na kikundi cha kigaidi cha Boko Haram, lakini
hadi sasa watu wanaendelea kuuwawa kinyama na kutekwa na Boko Haram.
Siku
ya Jumatatu, tarehe 10 Novemba 2014 zaidi ya wanafunzi 48 kutoka Chuo cha Ufundi,
kilichoko Kaskazini mwa Nigeria wameuwawa kikatili baada ya kulipukiwa na bomu la
kujitoa mhanga, wakati wanafunzi hao walipokuwa wamejipanga kwenye mstari, tayari
kuanza kuingia madarasani. Mji wa Potiskum ni maarufu sana kwa masuala ya uchumi na
biashara, Kaskazini mwa Nigeria, eneo ambalo limekuwa likiandamwa kwa mashambulizi
ya kigaidi yanayofanywa na kikundi cha Boko Haram.