Baraza la Maaskofu la Italia, CEI, Jumatatu lilianza Mkutano wake Mkuu wa 67 katika
kituo cha kiroho cha Assisi ambao unaendelea hadi Alhamisi Novemba 13.
Ujumbe
wa Papa Francisco kwa ajili ya Mkutano huu , ameonyesha ukaribu wake wa kiroho kwao
na kwa kanisa, akiwaombea Roho wa Mungu awajalie kama Wachungaji. Roho huyo , aweze
kulisha ubunifu na tumaini la Mkutano huo , ambao unalenga hasa katika kutazama kwa
kina maisha, malezi na utume wa kudumu wa Padre.
Aidha Papa ameutumia mkutano
huo kuwashukuru Maaskofu kwa dhati kwa utume wao mbalimbali wanaofanikisha kupitia
kutembelea Parokia , mihadhara, utoaji wa elimu kwa vijana, na familia, wagonjwa
majumbani na hospitalini, na kuwajali waliopungukiwa na watu maskini, bila ubaguzi.
Amewasifu kwa kufanya hivyo kwa uhuru wao kamili binafsi na bila malalamiko, wakitembea
pamoja katika upendo na wito wa Injili , na katika furaha iliyo ya kweli zaidi na
haki katika maisha ya udugu.
Ujumbe wa Papa unaendelea kueleza , kwa mkutano
huu kufanyika Assisi, kunamfanya apate hisia kali kwamba, ni Upendo Mkuu wa Mtakatifu
Francisco, uliolilishwa na Utakatifu wa hirakia ya utawala wa Mama Kanisa, na kwa
ajili ya makuhani. Na kisha Papa alikumbusha wajibu muhimu wa Maaskofu, katika kuimarisha
watumishi wa Kanisa, linaloundwa na watu wa Mungu, ambao kwa ushuhuda wao makuhani,
wametoa mchango mkubwa katika maisha yaliyowekwa wakfu. Na kwamba wameweza kujionea
mng’ao wa maisha ya waumini wakati wa mihadhara, majadiliano na watoto, kusaidia familia,
kutembelea wagonjwa nyumbani na hospitalini, kutunza maskini. Ujumbe wa Papa unaendelea
kusema Makuhani Watakatifu ni wale walio samehewa dhambi na kuwa vyombo vya msamaha,
wenye kujiweka daima katika mikono ya Yule ambaye ahadi yake haipungui na ufahamu
wao huongezwa na upendo kichungaji kwa watu waliokabidhiwa.
Ndiyo maana,
anaandika Papa - bado ni muda unaofaa kwa makuhani, kwa wakati huu, kujenga madaraja
ya kukutana kati ya Mungu na dunia. Kwa ajili hiyo, Papa Francisco pia alisisitiza
kwamba, haifai seminari, kuharakisha kutoa daraja la ukuhani kwa wale wanaowania
Maisha yaliyowekwa wakfu. Ni lazima kupima kwa kina, ukweli wa nia na malengo ya wale
wanaotaka kuingia katika maisha yaliyowekwa wakfu ,kuyatolea maisha yao kwa ukarimu,
katika hija ya maisha ya kumtumikia Yesu Kristo. Mafunzo, kwa hiyo, ni lazima kuambatana
na uzoefu wa uanafunzi wa kudumu, ambao hauna mwisho, kwa sababu makuhani kamwe hawakomi
kuwa wanafunzi wa Yesu. Kwa Papa Francisco, amesema, mafunzo ya awali na yale ya
kudumu yasiyokuwa na mwisho huwa na sehemu mbili za ukweli wa umoja unaoendelea katika
njia kudumu ya kuwa Padre mwanafunzi , katika upendo wa Mola wake.
Na
hivyo Papa anaendelea inakuwa ni tumaini katika kuiishi siku, inayoongoza katika
njia mpya ya kujifunza, majiundo ya kudumu na uwezo wa kuunganisha mitazamo mipana
ya kiroho na ile ya kitamaduni, na mwelekeo wa Jumuiya ya kichungaji, kama nguzo za
maisha thabiti ya kiinjili, yanayohitaji kudumishwa na nidhamu ya maombi ya kila
siku, huduma binafsi, unyenyekevu na ushuhuda wa kinabii; Maisha yaliyohuishwa upya
katika kanisa kwa uaminifu wa kuwekwa katika nafasi ya kwanza, miongoni mwa waamini.