Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu, aliwapokea Maaskofu wanaounda Baraza la Maaskofu
la mataifa kadhaa ya Afrika Magharibi, Senegal, Mauritania, Cape Verde na Guinea Bissau,
ambao wako katika ziara yao ya kila baada ya miaka mitano,” ad limina Visit”. Akizungumza
nao, Papa alionyesha kutambua kwamba, katika nchi hizi za Afrika Magharibi, ambako
mara nyingi Wakristo ni sehemu ndogo, bado hujitoa kwa ukarimu zaidi kwa ushujaa
wa kushuhudia Injili. Na hivyo inahitaji Maaskofu kufanya kazi ya ziada kupitia
majadiliano ya kujenga ushirikiano thabiti zaidi na Waislamu. Na kwamba, kukutana
nao , imekuwa ni nafasi kwake yeye na pia kwa Maaskofu hao kuimarisha kiungo cha upendo
kati yao na hasa kwa makanisa yao na kanisa la Roma.
Hotuba ya Papa , ilifanya
rejea kutoka katika waraka wake wa Injili ya Furaha, akiwahimiza Maaskofu kuendelea
kuhudumu utume wa Kanisa kama wainjilishaji waliojawa na Roho wa kuinjilisha kwa sababu
Roho Mtakatifu pia ataendelea kuwaunganisha na kuwajaza na ujasiri wa kutangaza kwa
ushupavu Injili katika maisha yao ya kila siku na kila mahali. Papa alieleza huku
akionyesha kutambua mazingira magumu yanayokabili mabaraza yao katika maana ya lugha
ya kutumia, utamaduni na mapito ya kihistoria katika nchi zao. Papa alizungumzia
haja ya kwa walei ,katika majimbo yao , kupokea mafundisho thabiti na roho ya majiundo
kwa ajili ya kutoa ushuhuda wa kuonekana kwa Kristo, katika mazingira ya jumuiya zao.
Injili ni lazima iingizwe katika maisha ya kijamii kwa misingi ya kiinjili. Imani
isipuuzwe katika maisha ya kijamii. Aliendelea kuwahimiza kwamba, zaidi ya yote
ya mizizi ya imani katika maisha ya watu, hasa katika kukabiliana na vitisho dhidi
ya mapendekezo ya kidini, na hasa katika kuzingatia maadili. Aliwataka Maaskofu
wasiongope kukemea mambo yanayoweza kuhatarisha maisha bora kwa jamii za Kiafrika,
ambayo kwa sasa inakabiliwa kutokana na uzushi wa malimwengu.
Papa Francisco
aliendelea kuelekeza mawazo yake kwa familia, hasa katika mwanga wa majadiliano yaliyofanyika
katika Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya familia. Papa anasisitiza kuwa "familia ni
kiini ya msingi kwa jamii na Kanisa. Familia ni mahali ambapo, misingi ya imani,
kanuni ya msingi ya maisha ya jumuiya hufundishwa. Na ni ndani ya familia ambamo mara
nyingi huzaliwa ya miito ya kikuhani na Utawa, kwa ajili ya katika Kanisa. Aidha
Papa aliwataka Maaskofu waendelee kwa ushupavu zaidi na mjadala wa kujenga na mahusiano
bora na Waislamu, mazungumzo katika haja ya kuishi kwa amani na mshikamano. Wakati
huo huo, alionya, Kanisa lazima kushuhudia upendo wa Mungu kwa watu wote, bila "tofauti
za kidini katika hatua ya kijamii."
Francisco, alisifu juhudi zinazo fanywa
na Kanisa katika kudumisha amani katika mataifa mengi ya Afrika Magharibi, akionyesha
kutambua mchango wa Kanisa, katika maendeleo ya binadamu, afya na elimu. "Baadhi
ya Makanisa yako licha ya uchanga wake na umaskini wake, bado huwa na ujasiri katika
mawasiliano na ukarimu wa imani.