2014-11-11 08:16:07

Jengeni utamaduni wa watu kukutana na kushikamana ili kudumisha amani!


Jumuiya ya Kimataifa inafanya kumbu kumbu ya miaka 25 tangu kuanguka kwa Ukuta wa Berlin, kielelezo cha siasa za chuki na ubaguzi, mwaliko kwa watu wa kizazi hiki kujitahidi kushiriki katika mchakato wa ujenzi wa madaraja yanayowaunganisha watu badala ya kuendeleza kuta zinazowatenga watu!

Baba Mtakatifu Francisko, wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana, Jumapili tarehe 9 Novemba 2014 kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, aliwaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema kusali na kumwomba Mwenyezi Mungu ili aweze kuwasaidia kujenga utamaduni wa watu kukutana.

Katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii na watu wote wenye mapenzi mema, Baba Mtakatifu anakazia kwa namna ya pekee, utamaduni wa watu kukutana, kushikamana na ujenzi wa amani.







All the contents on this site are copyrighted ©.