Kamwe Mkristo usiwe chanzo cha kashfa, lakini daima mtu wa kusamehe, na mtu wa imani.
Kila Mkristo, katika kila njia ya wito wake katika utendaji wa maisha ya kila siku,
anapaswa kutanguliza kusamehe na kamwe si kusababisha kashfa, kwa sababu "kashfa huharibu
imani." Papa Francisko ameonya wakati akiongoza Ibada ya Misa mapema Jumatatu hii
, katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta ndani Vatican.
Papa alieleza na kurejea
maneno ya Yesu kwa wanafunzi wake ambamo alionye heri kujifungia jiwe shingoni na
kujitupa bahari kuliko kuwakosesha wadogo hawa. Homilia ya Papa Francisco ilienga
katika somo la Injili ya Luka, ambamo kuna maneno matatu muhimu: dhambi, msamaha
na imani. Ole wao hao wanaowakosesha wengine anaonya Kristo. Na pia Mtume Paulo
alivyomwandikia Tito, anatoa maelekezo sahihi juu ya jinsi ya kutembea katika njia
ya maisha ya kikuhani. Si kuwa mtu wa vurugu, lakini mtu wa kiasi kwa kila jambo,
na wabwabwajikaji na mtu wa kuzua kashfa. Na hili si kwa makuhani tu lakini kwa Wakristo
wote. Aliendelea kutaja mifano ya kukashfu imani, akisema kama yule mtu anaye
jiita Mkristo, katika kusema na katika kukiri njia ya maisha, lakini ndani mwake
haamini chochote na maisha yake yako nje ya Ukristo. Hii inakuwa ni kashfa kwa sababu
hakuna kinachoshuhudia imani anayokiri. Pia mfano wa Mkristo au Wakristo, ambao
huenda kanisani, kwenda kusali, lakini hawayaishi maisha ya Kristo, bali huyagandamiza,
huko pia ni kuikashfu imani. Na pia kuwa wengine ambao husema, mimi siendi Kanisani,
wanaume au wanawake wanao heri kubaki nyumbani kuwa kama hao wanaokwenda kanisa lakini
kisha wakitenda ovyo kwa hili au lile, kama vile si wabatizwa. Hii ni kashfa kubwa
inayo haribu imani! Na ndiyo maana Yesu alisema kwa nguvu: jihadharini! Na hata leo
hii ni vyema kurudia maneno hayo, Jihadharini, kwa kuwa sote ni dhaifu katika kusababisha
kashfa.
Na kumbe sote tunapaswa kujua jinsi ya kusamehe mapungufu ya wenzetu
na kusonga mbele pamoja ktiakmwendo wa imani. Ni kusamehe daima, Papa alisisitiza,
kama Yesu alivyosema, zaidi ya mara saba kwa siku wakati tunadhulumiwa.Hapo Kristo
alionyesha maana na umuhimu wa kusamehe, hivyo Mkristo asiyeweza kusamehe , huyo
si Mkristo.
Kusamehe ni Sala ya Bwana, aliyofundisha na Yesu mwenyewe.
Papa alionya, si rahisi sisi kuelewa katika mantiki ya kibinadamu. Mantiki ya binadamu
hutoongoza katika nia za kutotaka kusamehe, bali kujenga kisasi; chuki na mgawanyiko.
Papa alieleza na kuhoji ni familia ngapi zimevunjika, au watoto kutengwa na wazazi
wao, waume na wake, kwa sababu za kutosamehe?.... Ni muhimu kufikiria hili kwamba,
kusamehe si kupoteza haki, lakini kuna maana ya kukubali kwamba Mungu pia ananisamehe
mimi kwa makosa yangu. Hivyo sisi sote yatupaswa kulielewa hili. Papa Francisco alieleza
na kuongeza bila shaka sasa tunaelewa kwa nini wanafunzi wa Yesu waliposikia maneno
haya ya kusamehe kutoka kwa Bwana, waliongeza imani yao.
Daima ni Kukumbuka,
haiwezekani kujiepusha na kashfa na kuwa mtu wa kusamehe bila kuwa mtu wa imani. Ni
tu kwa mwanga wa imani, ile imani tumepokea kutoka kwa Baba mwenye huruma, Mwana ambaye
alitoa maisha yake kwa ajili yetu, Roho wake anayeishi ndani mwetu , hutusaidia kukua
katika imani, ndani ya imani ya Kanisa, imani ya watu wa Mungu, waliopokea ubatizo
na kutakatifushwa. Na hii ni zawadi. Imani ni zawadi inayotoka kwa Mungu, aliyo
wamwangia mitume wa Yesu , walioomba:“tuongezee imani” .