2014-11-10 09:05:29

Papa: Tunahitaji kujenga madaraja si kuta


Mahali ambapo kuna moyo uliojifungia, maana yake kuna ukuta. Tunahitaji madaraja, si kuta! Ni maneno ya Papa Francisco , siku ya Jumapili adhuhuri kwa mahujaji na wageni waliokuwa wamekusanyika katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, kusali pamoja naye sala ya Malaika wa Bwana. Katika hotuba yake hiyo fupi, Papa alijiunga na dunia kukumbuka kuangushwa kwa Ukuta wa Berlin Novemba 9 1989.

Katika maadhmisho haya ya kupita miaka 25 tangu ukuagushwa kwa ukuta wa Berlin, Papa aliltaja kuwa ni tukio la kihistoria, kw aukuta huo ambao leo hii, ukuta imekuwa ni ishara ya mgawanyiko wa kiitikadi wa Ulaya na dunia kwa muda mrefu ulio tenganisha wakazi wa mji wa Berlin mara mbili.

Baba Mtakatifu aliendelea kuzitaja juhudi za kimyakimya za muda mrefu na kipindi kigumu cha mateso kwa watu waliopigana kwa ajili hii, lakini bila kukata tamaa wakiomba nguvu za Mungu na kuteseka, na baadhi hata kutoa sadaka maisha yao. Katika maadhimisho ya historia hii ya kuangushwa kwa ukuta wa Berlin, hatuwezi kusahau juhudi zilizofanywa na Mtakatifu Yohana Paulo II.

Papa Francis kisha alisali, ili kwamba kwa msaada wa Mungu, wanaume na wanawake wenye mapenzi mema waendelea kueneza utamaduni ya kukutana, kwa lengo la kuagusha chini za kiroho , ambazo bado zinaleta mgawanyiko duniani. Na pia aliomba ili kwamba kusiwe na mauaji zaidi na mateso ya watu wasio na hatia na ya wale waliouawa kwa sababu ya imani za kidini.

Kabla sala ya Malaika wa Bwana Papa Francisco pia alilikumbuka majitoleo ya Kanisa Kuu la Yohana wa Lateran la hapa Roma akisema , ni Kanisa Kuu la Roma, ambamo kitamaduni huitwa Kanisa Mama kwa Jimbo la Roma. Aliendelea kukumbusha majitolea ya kanisa hili, akisema, ni ukweli muhimu kwamba, hekalu hili lililojengwa kwa matofali ni ishara ya Kanisa hai na tendaji , “hekalu la kiroho

Aliongeza, jengo hili la kiroho, jumuiya ya watu walio takatifushwa kwa damu ya Kristo na kwa Roho ya Bwana Mfufuka , inatutaka sisi, kila mmoja wetu kuwa thabiti katika kushikilia zawadi ya imani na katika kutembea kwenye hija ya ushuhuda wa Kikristo. Na wakti huohuo akaonya kwamba , hili si jambo jepesi.

Papa Francisco alihitimisha kwa kusema, Sikukuu hii ya Kanisa Kuu la Laterani, inatualika "kutafakari juu ya ushirika wa makanisa yote," na kwamba kufanana kwa jumuiya hii ya Wakristo,kunahimiza sisi kujitahidi ili kwamba ubinadamu uweze kushinda vikwazo na uadui na kutofautiana, kwa kujenga madaraja ya uelewano na mazungumzo yanayoweza kuwabadili binadamu wote na kuwa familia moja ya watu wenye mapatano na mshikamano wa kidugu.








All the contents on this site are copyrighted ©.