Baba Mtakatifu Jumamosi hii amekutana na Maskauti Katoliki wa Italia , ambao kwa sasa
ni watu wazima, waliombelea kama sehemu ya maadhimisho ya Sikukuu yao ya kutimia
miaka 60 tangu kuanzishwa chama cha Maskauti Katoliki cha Italia. Katika hotuba
yake kwa Maskauti hao, Papa alitoa shukurani zake za dhati kwa kazi yao ya miaka
sitini ambamo wameweza kuonyesha ushuhuda wa kitume katika Kanisa na katika jamii,
maadili ya uaminifu, udugu na upendo kwa Mungu na jirani. Papa aliendelea kuwataka
waendelee kutembea katika njia hiyo, na kwa matumaini ya baadaye. Jumla ya wanachama
7000, Wakiwakilisha Maskauti watu wazima, nchini Italia, walipokelewa na Papa katika
Ukumbi wa Paulo VI. Chama hicho kilianzishwa mwaka 1954 na Mario Mazza. Shamra shamra
za mkusanyiko huo zilipambwa kwa nyimbo na shuhuda. Ilikuwa ni kanisa linalo toka
na kwenda nje kuhudumia kama Papa Francisco anavyopenda kanisa liwe. Rais na
Katibu wa Kitaifa kwa chama hiki kinachojukana kama Masci, alisema wanapenda daima
kuwa mashahidi wa ushupavu, wasiokuwa na woga wa kuingia ndani kwa ajili ya kuifikisha
imani . Kwa ajili hiyo, Papa aliwashukuru wote na kuwaomba waendelee na wito huo,
katika safari yao, wakingoza katika njia ya kweli kwa familia, licha mahangaiko ya
kieleo, daima washikilie katika kuitafuta njia ya haki, wakitembea kwa utulivu daima
katika kuongoza njia!
Papa katika hotuba yake ametaja mazingira matatu muhimu
, nayo ni familia, kama kiini cha jamii, jamii ya upendo na maisha bora, katika
jinsi ya kuhusiana na wengine na dunia. Na kwamba inatakiwa kuzingatia hili tangu
hatua zake za kwanza za maisha. Na kwa vyama kama hiki, ambavyo hujifunza njia
za maisha na juu ya uchaguzi wa elimu, ni muhimu kuthibitisha kwamba, elimu ndani
ya familia ni kipaumbele cha kwanza katika uchaguzi. Na hivyo kwa Wazazi Wakristo,
utume wa elimu uweze kuchipuka kutoka katika sakramenti ya ndoa, ambamo ndani yake
mna kazi ya kuwalea watoto kama huduma ya kweli kwa Kanisa.
Ni kutengeneza
njia kwa mjibu wa maisha ya kiskauti. Kama wanafunzi wa Kristo, Papa anasema, tuna
kila sababu ya kulinda na kutetea zawadi tuliyopewa na Muumba, "tunatambua alama
yake kwa wenzetu walioumbwa kwa mfano na sura yake.
Papa aliendelea kueleza
kwamba , tunaishi katika mashinikizo mengi ya mazingira na asili,lakini kama maskauti
wanavyotenda , haionyeshi tu kujiheshimu wao wenyewe lakini pia ahadi ya kuchangia
vyema na kuondoa yale yanayoichafua jamii inayokuwa na mwelekeo wakutaka kuyaangamiza
yaliyo mema kwa jamii , na pia katika kujitolea kwao katika mahitaji ya kijamii.
Papa alikamilisha hotuba yake kwa Maskauti na wito wa kuwa chachu ya kwa ajili
ya utambuzi wa mema ya kawaida na kuonyesha kama dira, "moyo ulioelekezwa kukutana
na hisia ya Mungu. amesema , katika utata wa kitamaduni kwa jamii ya leo, kushuhudia
kwa unyenyekevu, kwa ajili ya kuonyesha unyenyekevu upendo wa Yesu kwa watu wote,
na uaminifu wa wakristo katika huduma zao, inaweza kuwa ni chachu kwa wale waliopoteza
upeo wa kuona uwepo wa Mungu. Ni muhimu kuwa dira ya kweli ya maisha kwa wake na
waume, katika kuuleta karibu moyo, moyo unaokuwa na mwelekeo mpya katika hisia za
kukutana na Mungu.