2014-11-06 12:00:44

Askofu Beatus Kinyaiya ateuliwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Dodoma, Tanzania


Baba Mtakatifu Francisko amelipandisha hadhi Jimbo Katoliki la Dodoma na kuwa Jimbo kuu la Dodoma litakalojumuisha majimbo ya Singida na Kondoa. Baba Mtakatifu amemteua Askofu Beatus Kinyaiya kuwa Askofu mkuu wa kwanza wa Jimbo kuu la Dodoma, Tanzania. Kabla ya uteuzi huu, Askofu Kinyaiya alikuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki Mbulu.

Jimbo kuu la Dodoma lina Parokia 32 zinazohudumiwa na Mapadre wa Jimbo 41, Mapadre Watawa 39. Kuna Watawa wa kiume 92 na Watawa wa Kike 305 wanaofanya utume wao katika medani mbali mbali za maisha Jimbo kuu la Dodoma.

Askofu mkuu mteule Beatus Kinyaiya alizaliwa kunako tarehe 9 Mei 1957 huko Shimbwe, Jimbo Katoliki la Moshi. Baada ya masomo na malezi yake ya kitawa, akaweka nadhiri kunako tarehe 5 Juni 1988. Tarehe 25 Juni 1989 akapadrishwa. Tarehe 22 Aprili 2006, Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI akamteua kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Mbulu na kuwekwa wakfu tarehe 2 Juni 2006 kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Mbulu.







All the contents on this site are copyrighted ©.