2014-11-04 12:03:21

Askofu Christopher Kakooza ateuliwa kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Lugazi, Uganda


Baba Mtakatifu Francisko amekubali ombi la Askofu Matthias Ssekamanya wa Jimbo Katoliki Lugazi kung'atuka kutoka madarakani kadiri ya sheria za Kanisa namba 401, Ibara ya 1. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteua Askofu msaidizi Christopher Kakooza kutoka Jimbo kuu la Kampala, Uganda, kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Lugazi, Uganda.

Itakumbukwa kwamba, Askofu Christopher Kakooza alizaliwa kunako tarehe 15 Novemba 1952 hujko Lusaze, Uganda. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapadrishwa kunako tarehe 3 Juni 1983. Tarehe 2 Januari 1999, akateuliwa na Papa Yohane Paulo II kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Kampala, Uganda na kuwekwa wakfu hapo tarehe 17 Aprili 1999.







All the contents on this site are copyrighted ©.