2014-11-01 14:30:28

Siku ya Watakatifu wote, hutukumbusha kifo si mwisho wa maisha yetu


Katika maadhimisho ya Siku Kuu ya Watakatifu wote, Novemba Mosi, Baba Mtakatifu nyakati za adhuhuri, amehutubia umati mkubwa wa watu waliokuwa wamekusanyika katika uwanja wa Kanisa Ku la Mtakatifu Petro, Vatican, pia wakiwepo washiriki wa mbio za Watakatifu wote.

Katika hotuba yake amekumbusha kwamba, siku hizi mbili za kwanza za Mwezi Novemba, kwetu sote kama waamini , ni wakati wa kutoa maombi na tafakari juu ya mwisho ya maisha ya hapa duniani. Na ukweli wake, maadhimisho ya siku hizi mbili hukumbusha yote mawili , Watakatifu na Waamini Marehemu, wakionyesha maisha ya kanisa kuwa katika hija kama ilivyo elezwa katika Liturujia ya siku, kuwa ni dhamana ya kiroho inayo unganisha Kanisa na mbingu. Siku ya Watakatifu wote, ni siku ya kumtukuza Mungu kwa ajili ya wanaume na wanawake Watakatifu wa umri wote, na kariba zote ambao waliofikia mwisho wa maisha ya dunia, lakini walianza maisha mapya kwa Mungu. Wakati huo huo tunawakumbuka wapendwa wetu Marehemu, kwa kutembelea makaburi, chanzo cha faraja kubwa, katika kufikiri kwamba, wao wameungana na Bikira Maria, mitume, mashahidi na watu wote wa Mbinguni!

Papa aliendelea kusema, Maadhimisho ya Sikukuu hii ya Watakatifu wote, hivyo husaidia sisi kufikiria ukweli msingi wa imani ya Kikristo tunayokiri katika sala ya Nasadiki, Nasadiki katika ushirika wa watakatifu. Ni ushirika unatokana na imani inayo waunganisha walio wa Kristo kwa njia ya ubatizo wao. Ni muungano wa kiroho, usioweza kuvunjwa na kifo, lakini unaendelea katika maisha yajayo. Kwa kweli kuna dhamana isiyovunjika kati yetu, tulio bado katika dunia hii na wale ambao walivuka kizingiti cha kifo. Sisi hapa duniani, pamoja na wale ambao wameingia katika milele, huunda familia moja kubwa ya Mungu.

Ushirika huu mzuri kati ya mbinguni na duniani, unaodhihirishwa kwa kina zaidi katika maadhimisho hali ya juu na kina, katika Liturujia, na hasa katika maadhimisho ya Ekaristi, inayoeleza na kuonyesha muungano kamili kati ya wafuasi wa Kanisa. Katika Ekaristi, waamini wanakutana na Yesu aliye hai na nguvu zake, na kwa njia yake huingia katika ushirika na udugu katika imani, wale ambao wanaishi nao hapa duniani na wale ambao wametangulia mbele katika maisha ya pili, maisha kutokuwa na mwisho. Ukweli huu wa ushirika hutuvika furaha, uzuri na udugu na wote wake kwa waume katika imani ambao hutembea pamoja kama waamini, wakisaidiana kutembea pamoja katika safari hii ya barabara inayoelekea mbinguni. Na ni faraja kujua kwamba, kuna ndugu wengine ambao tayari wametangulia uwinguni, wanaoomba kwa ajili yetu, ili kwamba kwa pamoja tunaweza kutafakari umilele wa utukufu na huruma ya Baba.
Papa Francisko aliendelea kusema, katika kusanyiko kubwa la Watakatifu, Mungu alipenda kutoa nafasi ya kwanza kwa Mama wa Yesu. Bikira Maria yuko katikati ya ushirika wa Watakatifu, kama mlezi wa kipekee wa Kanisa zima la Kristo. Kwa wale wanaopenda kumfuata Yesu kwa njia ya Injili, Bikira Maria huwaongoza kwa usalama, kwa kuwa yeye ni Mama aliye makini na mwenye kujali, ambaye tunaweza kumwekea kila nia yetu na matatizo yetu.
Papa alieleza na kukamilisha kwa kuwaalika wote kumwomba Malkia wa Watakatifu wote, atusaide kutoa jibu kwa ukarimu na uaminifu kwa Mungu, anayetuita kuwa watakatifu kama yeye alivyo Mtakatifu (tazama Law 19.2; Mt 5:48).
Baada ya sala ya Malaika wa Bwana , Papa Francisco pia alitoa mwaliko kwa wote kuombea Mji Mtakatifu wa Yerusalem, na kwa ajili ya Waamini wa dini kuu tatu , Waislamu Wayahudi na Wakristo, ambao katika siku hizi wamekuwa ni mashahidi wa hali za mivutano na wasiwasi, ili waweze kuashiria amani, Mungu anayopenda kuiona katika familia zote. Pia alirejea tukio la kutangazwa kuwa Mwenye Heri Padre Pedro kama shahidi wa imani , huko Hispania. Na pia aliwataja na kuwatakia mema, wale wote walioshiriki katika mbio za Watakatifu wote, ambazo huandaliwa na Chama cha Don Bosco hapa Roma.








All the contents on this site are copyrighted ©.