2014-11-01 10:25:18

Orodha ya Makardinali na Maaskofu waliofariki dunia katika kipindi cha mwaka 2013- 2014


Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu, tarehe 3 Novemba 2014 majira ya asubuhi anatarajiwa kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, kwa ajili ya kuwakumbuka na kuwaombea Marehemu Makardinali na Maaskofu waliofariki dunia katika kipindi cha mwaka 2013- 2014. Katika kipindi hiki, Mama Kanisa amewapoteza Makardinali 10 na Maaskofu 111. Bara la Afrika limempoteza Kardinali Bernard Agre, Askofu mkuu mstaafu wa Jimbo kuu la Abijan, Pwani ya Pembe na Maaskofu 16.

Ifuatayo ni orodha ya Maaskofu waliofariki dunia kutoka Barani Afrika:

1. Askofu mkuu Matthias N'gartèri Mayadi, Jimbo kuu la N'Djamena, Chad
2. Askofu Zèphyrin Toè, askofu mstaafu Jimbo la Dèdougou, Burkina Faso.
3. Askofu Deogratias M Byabazaire wa Jimbo la Hoima, Uganda.
4. Askofu Pius Suh Awa, Askofu mstaafu Jimbo Katoliki la Buèa, Cameroon.
5. Askofu mkuu mstaafu Lawrence P. Henry, Jimbo kuu la Cape Town, A. Kusini.
6. Askofu mstaafu Fortunatus M. Lukanima wa Jimbo la Arusha, Tanzania.
7. Askofu mkuu mstaafu Boniface Lele wa Jimbo kuu la Mombasa, Kenya.
8. Askofu mkuu mstaafu Robert Dosseh-Anyron, Jimbo kuu la Lomè, Togo.
9. Askofu mstaafu Boniface N. Dalieh, Jimbo Katoliki la Cape Palmas, Liberia.
10. Askofu mkuu Damiao A. Franklin, Jimbo kuu la Lianda, Angola.
11. Askofu Joseph Befe Ateba, Jimbo Katoliki la Kribi, Cameroon.
12. Askofu mstaafu Pedro L. Antonio, Jimbo Katoliki la Kwito-Bie, Angola.
13. Askofu mstaafu Morkos Hakim, wa Jimbo la Sohag, Misri.
14. Askofu mstaafu Simon A. Okafor, Jimbo Katoliki la Awka, Nigeria.
15. Askofu mstaafu Joseph A. Gasi wa Jimbo laTombura-Yambio, Sudan ya Kusini.
16. Askofu mstaafu Louis Nganga A. Ndzando, Jimbo Katoliki la Lisala, DRC.







All the contents on this site are copyrighted ©.