2014-10-28 08:31:59

Ebola bado inatishia maisha Barani Afrika!


Shirika la Afya Duniani, WHO, linasema kwamba, ikiwa kama Jumuiya ya Kimataifa haitajifunga kibwebwe kupambana na maambuziki ya ugonjwa wa Ebola Barani Afrika, Mwezi Novemba, idadi ya wagonjwa wa Ebola inaweza kufikia watu elfu kumi kwa juma. Hadi sasa takwimu zinaonesha kwamba wagonjwa wa Ebola wamefikia 4, 922. Wafanyakazi wanaotoa msaada kwa wagonjwa wa Ebola Barani Afrika ndio wanaonesha wasi wasi mkubwa wa kuambukizwa na virusi hivi, kiasi cha kuwakatisha tamaa.

Wataalam wa afya wanasema, wananchi wanapaswa kuzingatia taratibu na kanuni ambazo zimewekwa na Jumuiya ya Kimataifa ili kuhakikisha kwamba, ugonjwa wa Ebola unadhibitiwa, kwani kwa sasa unaendelea kuwa ni tishio kwa watu wengi, kiasi hata cha kuhatarisha shughuli za kiuchumi na kijamii. Haki msingi za wagonjwa wa Ebola zinapaswa kuzingatiwa na kuheshimiwa, kwani kuna baadhi ya wagonjwa wa Ebola wamelalamika kwamba, wanabaguliwa na kutengwa.







All the contents on this site are copyrighted ©.