2014-10-27 15:32:00

Imani ya Kikristo ni mzizi wa kiroho Ulaya


Ulaya kwa nyakati hizi inahitaji roho ya unyenyekevu wa karama za kibenedikitine, ni maelezo ya Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin, wakati akiongoza Ibada ya Misa katika Monesteri ya Montecassino, kwa ajili ya adhimisho la 50 la kutangazwa kwa Mtakatifu Benedikto, kuwa msimamizi Mkuu wa Ulaya na Papa Paulo VI.

Kardinali aliikumbuka historia ya Papa Paulo VI, akisema, aliithamini kwa moyo mkuu, Monesteri ya MonteCassino,kama dhamana maalum kwake, ikijionyesha kwamba, tangu akiwa na umri mdogo , alijisikia kuwa na amani ya kweli ndani ya kuta za majengo ya monesteri, kazi na matunda na siri iliyofumbatwa katika karama za Mtakatifu Benedict. Na kwamba kuta thabiti, nzuri na utulivu, si tu vilikuwa ishara ya kuonekana kwa nje, lakini pia ni ishara ya fadhila ya amani ya ndani kama matokeo ya uaminifu kwa karama za Wabenediktini , katika upeo wa roho ya utu wa kimonaki wa Papa Paulo VI,uliyomsukuma miaka 50 iliyopita, baada ya misukosuko ya mashambulio ya kutisha ya Februari 1944, yeye mwenyewe kutabaruki Kanisa Kuu jipya la Montecasino na kumtagaza Mwenye Heri Benedict, kuwa Mtakatifu na msimamizi wa Ulaya.

Kardinali Parolin, aliendelea kueleza kwamba, Papa Paulo VI alikuwa na moyo wa kimonaki, daima akivutiwa na maisha ya kimonaki, ambamo aligundua uzuri wa sala. Ni katika hali ya ukimya na amani, Papa Paul VI, aliweza kupata majibu ya maombi yake, jibu la mtu kwa nyakati zake , lililohimiza haja ya kuwa katika ukimya wa Kibenedikitine. Kardinali ametaja ukimya huo kuwa na malengo mawili kwa ajili ya ujenzi wa Ulaya: nayo ni imani na umoja wa kiroho kwa watu wa Ulaya, vilivyo simikwa katika mafundisho ya injili.

Kardinali Parolin, anasema, Kama ilivyokuwa kwa Papa Paulo VI, Mtakatifu Benedict anakuwa ni mfano wa kuigwa, kwa sababu hii alikuwa ni mtu wa imani thabiti, na chombo cha umoja na uinjilishaji miongoni mwa watu mbalimbali: liyetumia ishara ya Msalaba, kitabu na jembe, kama msingi halisi kwa umoja Ulaya. Papa Paul VI alisema kuwa, pamoja na Msalaba, na sheria ya Kristo, Mtakatifu Benedict alisisitiza umoja wa kiroho na watu mbalimbali, katika kujisikia kuwa watu wa Mungu. Kwa Maandiko na udumishaji wa utamaduni, hudumisha mila na desturi za kale , kurejesha na kurutubisha ufahamu wa akili. Na hatimaye jembe, kama ishara ya utendaji wa kazi za kuinua ustawi wa mtu kwa juhudi zake mwenyewe kibinadamu.

Imani ya Kikristo – alisema Kardinali Parolin, imekuza ubinadamu, na kujitanua wenyewe kama mizizi wa kweli wa kiroho. Imani ya Kikristo ikiwa ni dhamana kubwa kwa Ulaya ya kale, lakini pia kwa nyakati hizi zetu na kwa siku za baadaye. Karama ya kimonaki, na urithi wake wa kiroho unaweza kweli kuchangia mazuri yote ya leo, ndani ya Ulaya na hata nje ya mipaka yake, na kusafisha njia kuelekea mshikamano wa binadamu. Ulaya ya kisasa, inahitaji unyenyekevu wa hali ya juu na ujasiri wa karama za Wabenediktini, katika kutambua ukuu wa Kristo na udumishaji wa sheria zake. Leo hii tunaweza kutangaza kwa watu wote utambuzi wa mizizi ya Kikristo katika bara la Ulaya, na kufikisha kwa wale waliopotea, habari njema ya kufanya mageuzi kupitia uzuri wa maombi na furaha, itokanayo na maisha ya kujitoa kwa Mungu.

Kardinali alikamilisha hotuba yake kwa kutaja hatua zilizo chukuliwa hivi karibuni, katika mtazamo wa kufanya upya Abasia ya Montecassino. Na alikumbusha yaliyoandikwa katika Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican na Barua binafsi ya Papa “Motu Proprio" Ecclesia Catholica "ya 1967, yenye kueleza wasiwasi wa kitume katika Abbasia, na hivyo kuhakikisha mfumo wa kisheria unaofaa zaidi kwa maisha ya kimonaki na kuhamasisha huduma ya kichungaji zaidi usikivu na mahitaji ya dunia ya leo. Na mwisho alitolea ombi kwa Mtakatifu Benedict, ili Ulaya iweze kurejesha maadili yake na kuwa na msukumo na nguvu mpya, katika kuzishughulikia changamoto za kisasa.








All the contents on this site are copyrighted ©.