Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania linatarajiwa kuwa ni mwenyeji wa mkutano mkuu
wa pili wa Makatibu wakuu wa Mabaraza ya Maaskofu kutoka katika Shirikisho la Mabaraza
ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati, AMECEA. Mkutano huu unatarajiwa kufanyika
katika mji mkongwe wa Bagamoyo, Jimbo Katoliki la Morogoro kuanzia tarehe 21 hadi
tarehe 22 Oktoba 2014.
Mkutano huu utaongozwa na Padre Ferdinandi Lugonzo,
Katibu mkuu wa AMECEA ambaye anafafanua kwamba, Makatibu wakuu kutoka AMECEA watapembua
kwa kina na mapana mikakati ya utekelezaji wa maazimio yaliyotolewa na Mababa wa AMECEA
katika mkutano wao wa kumi na nane uliofanyika mjini Lilongwe, Malawi. Mkutano huu
unafutia mkutano mwingine wa Bodi tendaji ya AMECEA uliomalizika hivi karibuni.