Wema na huruma ni mambo yanayosukuma matendo ya Mungu na hivyo kumkirimia mwanadamu
uwezo wa kuyaelewa, kwani yanaonesha ule ukaribu wa Mungu katika maisha ya mwanadamu,
kama inavyojidhihirisha kwa njia ya Yesu Kristo, Neno wa Mungu aliyetwaa mwili na
kukaa kati ya watu. Hiki ni kielelezo cha upendo wa hali ya juu unaofumbatwa katika
Fumbo la Utatu Mtakatifu.
Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji
wa mitandao ya kijamii anabainisha kwamba, Mkristo anapaswa kuwa kweli ni mtu wa huruma,
kwani hiki ndicho kiini cha Injili.