2014-10-15 08:13:49

Kumekucha Msumbiji!


Zaidi ya wananchi millioni kumi kutoka Msumbiji, Jumatano tarehe 15 Oktoba 2014 wanashiriki katika uchaguzi mkuu wa Rais na Wabunge. Chama cha Frelimo kinakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa Chama cha Renamo kinachoongozwa na Bwana Alfonso Dhlakama. Bendera ya Frelimo katika uchaguzi wa mwaka 2014 inapeperushwa na Bwana Filipe Nyusi aliyekuwa Waziri wa ulinzi. Frelimo kimekuwepo madarakani, tangu Msumbiji ilipojipatia uhuru wake kunako mwaka 1975.

Ni matumaini ya wananchi wa Msumbiji kwamba, viongozi watakaochaguliwa watajikita zaidi katika kutafuta mbinu mkakati wa kuibua fursa za ajira pamoja na kuwa na mgawanyo bora zaidi wa rasilimali na fursa za kiuchumi zilizomo nchini humo. Watu wanatarajia kwamba, Msumbiji inaweza kuibuka kidedea katika masuala ya kiuchumi licha ya kinzani za kisiasa na majanga asilia yanayokwamisha juhudi hizi.







All the contents on this site are copyrighted ©.