Sinodi: Kanisa lina utume kama ule wa Yohana Mbatizaji kwa familia...
Kanisa lina utume kama ilivyokuwa kwa Mtakatifu Yohane Mbatizaji katika familia. Ni
maoni ya Kardinali Ferdinando Filoni, atakapo toa mchango wake kwenye Sinodi maalum
ya Maaskofu kwa ajili ya Familia. Ujumbe wake utalenga katika ziara yake alioifanya
kama mjumbe wa Papa Francesco katika nchi ya Irak,kuona hali halisi za ghasia na
vurugu, zinazowakumba Wakristo na makundi madogo madogo ya kidini.
Akihojiwa
na mwandishi wa Radio Vatikan, alisema kwamba: Jambo la familia nyingi za Irak zilizolazimika
kukimbia nyumba zao, au kukataa kuacha imani yao, ni ushuhuda tosha na mzuri katika
mtazamo wa imani. Wao wameshuhudia imani yao japokuwa na matatizo yaliyowakumba ya
kuacha nyumba na mali zao zote.
Anaendelea kwamba, jambo lilomshangaza sana
alipokuwa Irak ni kuwa familia hizi zilizobaki na umoja mahali popote walipokuwa wakikimbilia,
na hivyo kwamba anayofuraha kuiambia sinodi na watu wote juu ya ushuhuda na uzuri
wa familia za kikirsto nchini Irak.
Kuhusu jambo la talaka katika familia
na wengine kutaka kuolewa tena Kardinali Filoni alitoa mfano kwamba Jumapili wakati
wa homilia ya Papa alisema inabidi kujiweka katika fumbo la Yesu , kutafakari maisha
yake ,na kuangalia mwenendo wake ,kwa namna Kardinali Filoni anaongeza kwamba,
Yesu naye alikabiliana na jambo hili kwa uwazi , hali ambayo leo hii ipo , na wakati
mwingine imezua mambo makubwa, na ndipo Kardinali anajiuliza je Yesu angefanya nini,
je angejibu namna gani katika matatizo ya sasa?
Lakini alitumia mfano kwamba
, japokuwa Mtakatifu Yohane mbatizaji aliuwawa kwa ajili ya kutaka kubaki katika
mafundisho ya Mungu, katika mpango wa Mungu, kwani haikuwa haki Herode awe na mke
wa kaka yake, na kwamba , Mtakatifu Giovanni hakufurahishwa na hali hiyo.
Herode
alitambua ukweli wa Yohane japokuwa Yohanne baadaye alilipa kwa maisha yake. Kardinali
alisema, ujumbe huo ni wa Yesu .Kanisa lina utume kama wa Yohane Mbazaji katika familia,
kwani ni kuelekeza kwa Kristo na kumtangaza Kristo.
Kardinali Elio
Sgreccia:Sheria ya asili kutokueleweka . Katika maelezo juu ya familia
naye Kardinali Elio Sgreccia Rais mstaafu wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Utetezi
wa Maisha alipata ya kusema alipokutana na mwandishi wa habari wa Radio Vatikana
kwamba, kueleweka vibaya kwa sheria ya asili ya maadili inatokana na ukweli wa ulimwengu
uliobadilika ,kwani jambo la uumbaji ni Mungu anayeumba vitu vyote , Mungu anayeumba
hata hali ya msingi ya maisha yetu. Lakini pia sisi tuko huru na tunahusika kwa sababu
kuna hali inayoruhusu, ni hali yetu ya kiroho na kimwili ambavyo vimeungana wa pamoja.
Mwili na roho ni sehemu ya asili ambayo imetanda mizizi ya uumbaji lakini
sehemu hiyo ya asili ya maisha inapuuzwa , ambayo ilianzishwa na Mungu katika uumbaji
, na imekuwa na ugumu wa kutambua thamani yake ya asili na kila mmoja kuielewa anavyotaka,
alisema Kardinali. Kwa namna hiyo aliongeza inahitajika huduma ya kichungaji kuangaza
vizuri ukubwa na mshangao, wa uzuri wa wito wa kikristo katika familia , na ndoa
kama ukamilifu hai, wa kukamilisha upendo wa kibinadamu na mapendo ya Mungu
Ni
lazima kupendekeza Katekesi ambayo siyo fupifupi kama ya watoto wadogo bali katekesi
endelevu .Kardinali aliongeza kwamba, muda umefika wa kuanza habari mpya ya uinjilishaji
bora, ambo utasindikiza katika maisha yote na kuwafikisha katika ukomavu. Kardinali
anafikiria kwamba ndoa nyingi zinavunjika , kabla ya kutambua ni nini maana ya ndoa
labda ni kwasababu haifanyiki katekesi halisi ya mada ya ndoa.