Papa afungua Sinodi Maalum ya Maaskofu kwa ajili ya familia
Baba Mtakatifu Francisko, Jumapili hii 5 Oktoba, 2014, aliongoza Ibada ya Misa Katika
Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican, kwa ajili ya kufungua Sinodi Maalum ya Maaskofu
juu ya familia. Katika Homilia yake Papa, ametafakari Neno la Mungu kutoka katika
Kitabu cha Nabii Isaya kuhusu shamba la Bwana na ndoto yake. Ameeleza Mpango wa
Mungu na upendo wake ni kwamba; wakulima watunze shamba la mizabu, kwani mizabibu
ni mmea ambao unahitaji huduma.
Papa aliendelea , kwa hiyo ndoto yake Mungu
kwa ajili ya watu wake, ni kwamba Yeye anapanda na kulitunza kwa upendo na kwa subira,
ili watu wapate kuwa watakatifu na ambao wanaweza kuleta matunda.
Katika
unabii wa zamani na katika mafundisho ya Yesu mara nyingi ndoto ya Mungu imesumbuliwa.
Kwa sababu katika kitabu cha Isaya inaonyesha kwamba japo shamba la mizabibu lilitunzwa
kwa upendo mkuu lakini lilitoa matunda mabichi na yenye uchachu (Is 5,2.4), Wakati
Mungu alikuwa anasubiri kupata haki yake, matokeo ilikuwa ni kumwagika damu, alisubiri
haki yake, akasikia yowe.
Kwa upande wa Injili Papa anaelezea kwamba ni
wakulima ambao waliharibu mpango wa Bwana, wao hawakufanya kazi , bali waliwaza mipango
yao inayowahusu.
Katika msemo wa Yesu anawambia wakuu na makuhani, wazee wa
watu , kwa maana hiyo wenye busara, ni hao ambao Mungu aliwakabidhi ndoto yake,ya
shamba ili walime na kulitunza, isishambuliwe na wanyama mwitu.
Papa alisema
, hiyo ndiyo kazi ya wakuu wa watu, kulima shamba la mizabibu kwa uhuru, na kujishughulisha.
Yesu anaonyesha kwamba wale wakulima ambao walitawala shamba la mizabibu kwa najivuno
na kwa pupa waliamua kuondoa hata uwezekano wa Mungu kukamilisha ndoto yake kwa watu
alio wachagua.
Kishawishi cha pupa , Papa aliongeza, kipo daima kwa maana
hata katika maelezo ya nabii wa Ezekieli kwa wachungaji, ambao Mtakatifu Agustino
aliongelea katika masifu ya jumapili juu ya pupa ya fedha na utawala. Katika kutosheleza
pupa hiyo wachungaji wabaya waliwatwisha mizigo mizito isiyochukulika ambayo hata
wakuu hao wasingeweza kuinyanyanyua kwa kidole chao(Mt 23,4).
Papa alisema
kwamba katika Sinodi ya maaskofu hata wao wanaitwa kufanya kazi katika shamba la
mizabibu la Bwana. Mkutano wa Maaskofu siyo wa kujadili mawazo mazuri na ujanja, au
kutazama nani mwenye akili zaidi. Lakini ni mikutano kwa lengo la kusaidia kulima
na kutunza vema shamba la Bwana, kwa mshikamano wa ndoto yake, kwa ajili ya mpango
wake wa upendo juu ya watu wake.
Papa anabainisha kwamba kwa namna hiyo Bwana
anawaita kutunza kwa uangalifu familia ambayo tangu asili yake ni sehemu ya ishara
yake ya upendo kwa binadamu .
Wote tu wadhambi, aliongeza Papa kwa sababu
hata sisi inawezekana tukawa na kishawishi cha kutaka kutawala shamba kwa sababu
ya pupa ambayo haikosekani katika maisha ya binadamu.
Ndoto ya Mungu daima
inakumbana na unafiki wa watumishi wake, lakini inawezekana kufaidi ndoto ya Mungu
iwapo tutaongozwa na Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu anatupatia busara ambayo ni
zaidi ya sayansi, kwa ajili ya kufanya kazi kwa ukarimu na kwa uhuru wa kweli na
kwa unyenyekevu kiutendaji.
Papa alimalizia kwa kuwaomba Mababa wa Sinodi,
walime na kutunza vema shamba, kwani inabidi mioyo yao na akili zao zijazwe Amani
ya Mungu inayozidi akili zote. Wawe ndani ya Yesu kristo kama asemavyo Mtakatifu Paulo
Fil 4, 7. Kwa namna hiyo mawazo yao, mipango yao ifananane na ndoto ya Mungu, ili
kuunda watu wake watakatifu wanaotoa mtunda ya ufalme wa Mungu (Mt 21,43)