2014-10-02 09:07:33

Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Kipapa la Haki na Amani


Jumatano 1 -3 Octoba ulianza mkutano wa mwaka wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Haki na Amani, kwa lengo la kujadili Waraka wa Kitume wa Papa juu ya Furaha ya Injili (Evangelii Gaudium ) ambapo Papa Francisco alifunga nao mwaka imani. Waraka huu umeleta hamasa mpya katika shughuli za Baraza la kipapa la haki na amani.
Pamoja na mada muhimu kwa shughuli za Baraza la kipapa la Haki na amani na shughuli za jamii katika nchi zilizo na hali za ghasia na migogoro, wawakilishi wa nchi hizo wataHudhuria mkutano huo wa mwaka.
Vilevile watagusia mada ya maadhimisho ya miaka 5 ya Waraka wa (Caritas in veritate) na maadhimisho ya miaka 10 ya maandishi ya Mafundisho ya kanisa.
Taarifa inasema kwamba watatafakari pia Waraka wa Upendo katika Ukweli "Caritas in veritate" na maandishi ya mafundisho ya kanisa, na uwezekano wa kusahihisha au kuboresha
Tarehe hiyo ya mkutano imependekezwa kwa lengo la kuwawezesha wajumbe husika kuhudhuria hata wale watakao hudhuria Sinodi maalumu juu changamoto ya familia katika mazingira ya uinjilishaji, itakayoanza tarehe 5-19 Octoba
Mkutano wa Balozi wa Papa katika nchi za Mashariki ya Kati na Viongozi wa Idara za Curia ya Roma.







All the contents on this site are copyrighted ©.