Epukeni malalamiko kama vile mko katika ukumbi wa sanaa, kwani wapo wanaoteseka kweli
(Vatican Radio) Kulalamika wakati wa kipindi cha giza ni sala lakini angalieni kuepuka
malalamiko kama wale walioko kwenye ukumbi wa sanaa, kwa ni wapo wenye shida za kweli
wanaostahili kulalamika kama vile wale wanaoishi katika majanga makubwa ya mateso
mfano Wakristo wenzetu waliofukuzwa katika makazi yao kwa sababu ya imani yao.
Ni homilia ya Papa Fransisko Jumanne 30 Septemba wakati wa Ibada ya Misa, ndani ya
Kanisa dogo la Mtakatifu Marta Vatican. Akichambua somo la kwanza kuhusu historia
ya Ayubu anayelaani siku ya kuzaliwa kwake , Papa alisema kwamba, aliwekwa katika
majaribu, kwani alipoteza familia yake yote, alipoteza utajiri wake wote , akapoteza
afya ya mwili wake, na ukawa ni vidonda tupu vya kutia kinyaa. Papa aliongeza, wakati
huo Ayubu alipoteza subira, na kusema maneno hayo ambayo siyo mazuri. Lakini yeye
alizoea kusema ukweli , na ndiyo maana muda huo alikuwa akisema ukweli, Papa aliuliza
swali je huyo mtu alikufuru? Mwanadamu huyo aliyechwa peke yake, je alikufuru?
Je
Yesu alipolalamika kwamba Baba kwanini umeniacha je alikurufu, ni fumbo hilo. Papa
alisema kwamba amesikia mara nyingi watu wanaishi katika hali ngumu , na ya uchungu,na
wamepoteza mengi na wanajisikia upweke, wameachwa , na kulalamika wakijiuliza kwa
swali hilo kwanini?, wanamkasirikia Mungu… Lakini Papa aliwataka waaamini waendelee
kusali hivyo, kwasababu swali hilo ni sala, kwa maana ilikuwa vilevile ni sala
hata Yesu alipomweleza Baba yake kwamba mbona umeniacha.
Sala ya Ayubu inajionyesha
kwamba kusali ni kuwa mkweli mbele ya Mungu, na Ayubu ilimpasa kusali hivyo kwa hali
yake, maana sala ya kweli ni ile itokayo rohoni kutokana na hali unayoishi, ni sala
wakati wa kipindi kigumu na cha shida, ni wakati wa maisha kama vile hakuna matumaini,
ni wakti si rahisi kuona upeo.
Aliongeza kwamba watu wengi leo hii wako
katika hali kama ya Ayubu, na ni watu wema kama Ayubu hawajui na hawajui kwa nini
hali hiyo imewatokea. Ndugu zetu kaka na dada hawana matumaini , ukifikiria majanga
na ghasia za wakristo wenzetu waliofukuzwa katika nyumba zao na kubaki bila kitu
chochote ,nao wanajiuliza, Bwana mimi nilikuamini, kwani kukuamini wewe ni kulaamiwa
Bwana?
Papa aliendelea kuwataka waamini wawafikirie wazee waliofukuzwa, wagonjwa,
na watu wengi wenye upweke mahospitalini, na kwa watu hao aliwataka wakumbuke kwamba
Kanisa linasali kwa ajili yao, na linateseka pamoja nao katika uchungu wa mateso
yao. . Papa kisha aliwageukia na swali wale ambao hawana ugonjwa, njaa,
shida ya mahitaji yoyote, wanapopata giza rohoni, je wanamwacha Mungu na kuacha
kusali? Kwani alibainisha kwamba wapo watu kama hao wanasema , nimemkasirikia Mungu
, siendi Misa tena je ni kwanini? Papa aliuza. Kwaajili ya kitu kidogo tu. Alitoa
mfano mmoja kuhusu Mtakatifu Teresa wa mtoto Yesu mwishoni mwa maisha yake , alipata
giza la namna hiyo rohoni akifikiria kuona mbingu ndani mwake, lakini aligundua kwamba
alikuwa anajidanganya na ndoto zake.
Papa Francisco aliendelea kwamba mara
nyingi tunajisikia katika hali hii na kuishi katika hali hiyo.Watu wengi wanajisikia
kuishi kama vile hawafanyi lolote. Lakini Mtakatifu Teresa alikuwa akisali na kuomba
nguvu ya kuendelea mbele katika giza hilo . Njia hiyo inaitwa subira . Kwani maisha
yetu, maisha ya wengi ni rahisi kuishi katika hali ya kulalamilka kama ulalamikavyo
umati wa watu waliokusanyika katika ukumbu wa michezo, wanapopatwa na matatizo kidogo..
Ni hali ya watu wengi ndugu zetu wanaoishi katika giza hata kupoteza matumaini. Wengi
wanaishi katika kilindi cha kujisahu wenyewe. Pia Yesu alipitia katika njia hiyo ,
katika mlima wa mizeituni hadi njia ya msalaba na kusema Baba mbona umeniacha.
Papa
Francesco alimalizia homilia yake akitoa maelekezo ya njia mbili za kufuata wakati
wa kipindi cha giza kwamba, kwanza ni kujiandaa na kipindi cha giza litakalokuja,
na pili kusali kama Kanisa linavyosali kwa ajili ya ndugu wanaoteseka kwenye bonde
la machozi katika kipindi hiki cha mateso, na ukosefu wa matumaini . Hiyo ndiyo sala
ya kanisa.