2014-09-30 09:26:22

Papa: Uzee ni kipindi cha Neema


Jumapili 28 Septemba katika uwanja wa Vatican, ulifurikwa na sura mbalimbali za wazee kutoka pande zote za dunia, ambako Papa Francisko alikutana na wazee kaka ilivyokuwa imeandaliwa na Baraza la Kipapa kwa ajili ya familia, kuadhimisha Siku Kuu ya Wazee, iliyoitwa ” Baraka ya maisha marefu”. Papa mstaafu BenediktoXV1, alikuwa miongoni mwao, ambapo Kabla ya adhimisho la Ibada ya Misa, Papa Francisko, alisikiliza baadhi ya shuhuda za wazee na pia kuongea nao.

Alimshukuru Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Familia, Askofu Mkuu Vincenzo Paglia kwa maandalizi haya ,vilevile alipongeza pia Papa Mstaafu Benedikito XV1 kwa uwepo wake, na kwamba, mara nyingi amefurahia kuona anaishi ndani ya Vatican. Amemwita kuwa babu mwenye hekima ndani ya nyumba. Papa Francesko ameshangazwa na ushuhuda wa wazee wawili kutoka Iraq walioweza kukimbia ghasia na vurugu, na kuita uwepo wao kuwa zawadi kwa kanisa.

Papa Francisko alisema, vurugu dhidi ya wazee na watoto siyo kitendo cha kiutu, lakini Mungu hawaachi wazee peke yao, huwapa msaada wake, ili waendelea kutoa kumbukumbu kwa ajili yao na kwa ajili yetu , kwa sababu ni sehemu ya familia kubwa ya kanisa. Imani yao ni kama mti unaoendelea kukua na kutoa matunda. Uzee ni kipindi cha neema ambamo Bwana anatualika katika wito wake, kutunza na kuonyesha Imani, anatualika kusali na hasa kuomba na kuwa karibu na wenye kuhitaji. Wazee wana uwezo wa kutambua hali ngumu , na nguzo yao ni sala ambayo ina nguvu, alisema Papa.

Papa aliendelea kuwaenzi babu na bibi kwamba, kwa namna ya pekee wamepokea baraka ya kuona watoto wao (Zab 128,6) na wao wamekabidhiwa kazi kubwa ya kuonyesha uzoefu wa maisha, historia ya familia katika Jumuiya ya watu. Babu ni “ Baba mara mbili”, na ndivyo ilivyo kwa bibi “mama mara mbili” Tukikumbuka wito wa babu wa kuendeleza thamani ya urithi wa Imani.

Papa Francisco kwa maneno hayo, alikumbuka ziara yake aliyoifanya hivi karibuni nchini Albania na nchi nyingine zinazofanana na hiyo kwa kipindi cha kidkteta ya kikomunisti, kwamba ni wazee waliofanya kubatiza watoto mafichoni , na hivyo kuokoa imani ya watu hao.

Kwa nyakati hizi Papa Francisko alibainisha kwamba siyo familia zote zinawapokea wazee, Na ndiyo maana ni vema kuwepo nyumba za kuwapokea , lakini ziwe nyumba ukweli na wala zisiwe mahabusu, nyumba hizo iwe kwa manufaa ya wazee na isiwe kwa manufaa mengine. Kwa mantiki hiyo Papa aliwashukuru kwa wale wote wanaokwenda kuwatembelea wazee katika nyumba za kupokea wazee, na wote wanatoa huduma kwao.Vile vile kwa vijana wengi wanao fanya kazi ya kuwafurahisha wazee wenye nyuso za masikitiko , kurejea furaha ya maisha katika umri wao mkubwa. Papa alisema kwamba kuna tatizo kubwa la kuwaacha wazee peke yao, akisema katika ukweli hii ni sawa na eutanasia iliyojificha.

Matatizo ya utamaduni wa ubaguzi dhidi ya watoto, vijana wasio kuwa na kazi, na wazee inasikitisha sana, hasa pale inapokuwa kwa sababu za mipango ya kiuchumi na maisha. Papa alitaja ubaguzi huo ni nje ya utu tena ni ubatili mtupu. Ni lazima kutanguliza utu na si fedha. Aliongeza na kumtaka, kila mkristo, kupinga sumu ya utamaduni wa ubaguzi, na kuunda jamii tofauti, inayokaribisha zaidi, yenye utu zaidi , na zaidi ya yote ambayo haiweki pembeni wadhaifu na wanyonge.

Watu wasio tunza wazee , ni watu wasiokuwa na maisha endelevu , kwa sababu wanapoteza kumbukumbu, na kupoteza mzizi: kila mkristo lazima atunze mzizi wa njia ya sala, neno la Injili na matendo ya huruma. Papa alimalizia akitoa mfano kwamba vitu vizuri katika maisha ya familia , na katika maisha ya binadamu ni kumbembeleza mtoto na kumwacha mtoto abembelezwe na babu na bibi.

Homilia ya Papa kwa wazee, imekuwa ni makutano yaliyojaa furaha ,amani na matumaini
Baba Mtakatifu Francsiko, baada ya kukutana na kubarizi na wazee, katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro , aliingia katika hatua nyingine ambamo aliongoza Ibada ya Misa ya shukurani kwa Mungu kwa majaliwa ya kukutana na wazee. Papa aliyaita makutano haya kuwa ni wakati uliojaa furaha, imani na matumaini.

Katika homilia yake , alikumbusha juu ya Mama Maria akiwa kijana, wakati huo binadamu yake Elizabeti alikuwa mzee , lakini kwa huruma Mungu katika uzee wao, Zakaria na Elizabeti , wakajaliwa mtoto. Kwa njia hii Mama Maria anatuonyesha njia , ya kwenda kukutana na wazee ndugu zetu, kukaa nao, kuwasaida, na zaidi kujifunza kutoka kwao , kwani wazee wana hekima na busara ya maisha.

Papa alieleza na kwa kuyarejea masomo ya Siku akianza na somo la kwanza, akisema, lilionyesha kana kwamba linaongelea juu ya amri ya nne ya Mungu, isemayo waheshimu baba na mama upate miaka mingi na heri duniani ambayo Bwana Mungu amekupatia (Kut 20,12) Hakuna maisha ya endelevu ya watu kama hakuna makutano na kizazi kipya , iwapo hakuna watoto wanaopokea ushuhuda wa maisha ya wazazi wao. Pamoja na shukrani za utambuzi kwa wazazi walio tupatia maisha haya, hatuna budi kumshukuru Baba Mungu aliye mbinguni. Aliongeza Papa.

Papa Francisco aliangalisha vijana wa kizazi hiki kwa sababu ya tamaduni na kwamba wanatofautiana na kizazi kilichopita, aliwataka wawe makini katika uhuru wa chaguzi, ni lazima kuutauta ukweli na siyo chaguzi potofu zinazoongozwa na uchu wa fedha, tamaa na madaraka.

Papa aliendelea kutafakari juu ya somo la pili kutoka waraka Mtakatifu Paulo wa Timotea, akiielekea jumuiya ya wakristo, kwamba Yesu hakutengua sheria katika familia , kati ya kizazi , bali alileta ukamilifu. Bwana aliunda familia mpya, ambayo imeungana kwa ajili ya kufanya mapenzi ya Mungu Baba. Upendo wa Yesu kwa baba yake unaleta ukamilifu wa upendo wa wazazi wake na, ndugu zake , babu zake na kurudisha upya ndani ya familia kiini cha Injili na Roho Mtakatifu. Kwa namna hiyo Mtakatifu Paulo anamsihi Timoteo ambaye ni mchungaji na kwa maana hiyo baba wa Jumuiya , kuwa na heshima ya wazazi na familia , na kumsihi pia awe na maelewano kama watoto. Babu ni kama Baba na bibi kama mama (1Tm 5,1).

Mapenzi ya Mungu ni kwa watu wote hata Mkuu wa Jumuiya, na zaidi ya hayo upendo wa Kristo unamsukuma afanye hivyo kwa upendo mkubwa. Kama vile Bikira Maria alivyofanya japokuwa aliitwa kuwa Mama wa Masiya, lakini anajisikia kusukumwa na upendo wa Mungu , ambamo ameupokea na kukimbia kumtembelea Elizabeti.

Ukirudi katika picha iliyojaa furaha ,imani, matumaini na upendo , unaweza kufikiria Bikira Maria akiwa nyumbani mwa Elizabeth, aliwasikia Zakaria na mkewe wakisali zaburi yenye maneno kama “Ee Bwana Mungu ndiwe tumaini langu tokea ujana wangu,… usinitupe wakati wa uzee wangu , nguvu zangu zipungukapo usiniache…Na hata nikiwa ni mzee mwenye mvi, Ee Mungu usiniache. Hata niwaeleze wat u wa kizazi nguvu zako, na kila atakayekuja uweza wako”. (71,5.9.18).

Kijana Maria alisikiliza , na yote akayaweka katika moyo wake, Hekima ya Elizabeth na Zakaria , imetajirisha moyo wa binti Maria; licha kwamba hawakuwa na uzoefu wa kuwa baba au mama, kwa sababu hata wao ilikuwa ni kwa mara yao ya kwanza, lakini walikuwa na ujuzi wa imani, ujuzi kwa Mungu , ujuzi katika matumaini yanayotoka kwa Mungu, na kwa namna hiyo ndiyo maana dunia inahitaji ujuzi huo kila wakati.
Maria alitambua manufaa ya kuwasikiliza wazazi wazee kwa hekima yao na ikawa tunu kwake katika safari yake kama mwanamke na kama mama. Papa alimalizia kwamba Bikira Maria anatuonyesha njia ya kukutana kati ya vijana na wazee. Msingi wa siku zijazo unategemea na kuhitaji hatua hiyo ya kukutana.Vijana wanawapa nguvu wazee katika safari ya maisha hati hatima yake, vilevile wazee kwa hekima zao huwatia nguvu vijana katika safari yao ya maisha.







All the contents on this site are copyrighted ©.