2014-09-25 16:07:18

Chuo Katoliki cha Mwenge sasa Chuo Kikuu Katoliki kamili


Kilichokuwa Chuo Kikuu kishiriki cha Elimu cha Mwenge Tanzania(MWUCE), kimepewa hadhi ya kuwa Chuo Kikuu Kamili, na Tume kwa ajili ya Vyuo Vikuu ya Tanzania (TCU). MWUCE kilikuwa ni Chuo mwambata kwa Chuo Kikuu Katoliki cha Mtakatifu Augustine Tanzania (SAUT).

Sista Bridgita S. Mwawasi, ssj, anaripoti kwamba, hii inamaanisha wanafunzi watakao sajiriwa katika Chuo Kikuu Kipya Katoliki cha Mwenge(MWUCAU) kwa mwaka wa masomo 2014/2015 wataingizwa na kufanya masomo yao, chini ya sheria mpya za Chuo Kikuu hiki (MWECAU). Hatua hii ni kubwa katika nyanja ya taaluma Tanzania.

Na kwamba, wakati wa uzinduzi wa mwaka mpya wa kitaaluma 20124/2015, tukio la Jumatatu Septemba 22, 2014, Askofu Isaac Amani, Mwenyekiti wa Bodi ya uongozi MWUCE na Askofu wa Moshi, alimtangaza Padre Dr Philbert Vumilia, kuwa Kaimu Makamu Mteule wa Chuo kikuu mpya.

Askofu Amani alisema kuwa mabadiliko ya MWUCE, kuwa Chuo Kikuu kamili ilikuwa ni hatua kubwa ya maendeleo kwa jamii nzima ya Mwenge, na macho ya jamii sasa yameelekezwa zaidi katika kuona uwajibikaji wa chuo hiki katika malengo yake. Na alitoa wito kwa wote, tangu utawala, wafanyakazi wa kitaaluma, wanafunzi na wadau wote, kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu zaidi, mkono kwa mkono, ili kuhakikisha mafanikio katika kuiendeleza jamii ya Watanzania kitaaluma.
Na kwa upande wake, Kaimu Makamu Mteule wa Chuo, Padre Dr. Philbert Vumilia aliishukuru Tume ya Vyuo Vikuu kwa ajili ya kuidhinisha MWUCE , kuingizwa katika hadhi ya chuo kikuu. Na pia aliwapongeza wote wakiwemo wafanyakazi na wanafunzi wa MWUCE kwa kuchangia mafanikio haya. Na aliomba roho hiyo ya kufanya kazi bila kuchoka kwa ajili ya kuhudumia Watazania na watu wa Mungu kwa ujumla,iendelezwe bila ukomo.

Dk Vumilia anatajwa akiwa mmoja wa wafanyakazi wa MWUCE, alifanya kazi bila kuchoka akishirikiana na wafanyakazi, wanafunzi, maaskofu na TCU kutimiza mahitaji ya TCU yaliyowezesha MWUCE kuwa Chuo kikuu cha MWUCAU,kama Chuo Kikuu Katoliki cha kujitegemea, kinacho jihusisha hasa na kutoa elimu ya juu chini ya miliki na usimamizi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania,(TEC).Chuo hicho kiko kaika viunga vya mji wa Moshi, Kaskazini Mwa Tanzania.

MWUCE ilianzishwa mwaka 2005 kama Chuo Kishiriki cha Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine Tanzania, SAUT. MWUCE ni mrithi wa Chuo cha Ualimu cha Mtakatifu Yoseph, kilichoanzishwa mwaka 2001 kwa ajili ya utoaji wa Stashahada katika Elimu kwa mafunzo walimu wa somo la Sayansi katika shule za sekondari.

Vyote viwili, Chuo cha Ualimu St Joseph na Taasisi ya Elimu ya Mwenge,walijitihadi kuutumia muda wao ,kufundisha na kujifunza, utafiti na huduma za jamii katika kufanikisha lengo la kutoa wataalamu walioiva vyema katika masuala ya kijamii na uwajibikaji kwa manufaa ya Watanzania na wengine kwa ujumla. Na hilo linaendelea kuwa lengo la jitihada za MWECAU kuendelea kutoa matunda bora na kuwa na shikamano thabiti na wadau wengine katika uwanja wa elimu kama chuo kikuu kikamilifu.








All the contents on this site are copyrighted ©.