2014-09-23 08:35:52

Tamko la Madhehebu ya Dini katika Mkutano wa UNO


Mkutano Mkuu wa 59 wa Umoja wa Mataifa unatazamiwa kufungulia 23Septemba mjini New York , unahudhuriwa na viongozi Wakuu wa nchi na Mawaziri kutoka nchi mbalimbali za dunia. Mkutano huo unahusu mabadiliko ya hali ya hewa.

Viongozi Wakuu wa madhehebu ya dini wametoa tamko litakalowasilishwa katika mkutano huo, likiwa na kaulimbiu:" hali ya hewa, Imani na Matumaini: Muungano wa tamaduni za dini juu ya umoja endelevu”.

Tamko hilo limesainiwa na viongozi wakuu wa madhehebu mbalimbali na kati ya viongozi hao 30, yupo Kardianali John Onaiyekani wa Abuja Nigeria, Kardinali Oscar Rodrigue Maradiaga wa Caritas Internationalis, Padre Michael Czerny S.J mwakilishi wa Baraza la Kipapa katika Tume ya Ushauri, haki na Amani.

Tamko hiili linasema kwamba Viongozi wawakilishi wa madhehebu mbalimbali ya dini wamekusanyika pamoja kuonyesha mshikamano wao pia wasiwasi walio unao kutokana na mabadiliko ya tabianchi, ambayo inaathiri ardhi ambayo mwanadamu amekabidhiwa aitunze.

Wanatambua kutokana na taarifa za kisayansi juu ya ukosefu na hatua madhubuti kuchukuliwa dhidi ya kukomesha mabadiliko ya tabia nchi. Kitendo hicho cha kutokuchukua hatua zinazostahili zinazidi kusababisha mabadiliko haya , na hivyo viongozi hawa wako tayari kufanya majadiliano na wanahusika na wale wasiotaka kutokujali suala hili.

Kutokana na vyombo vya habari , mitandao ya kijamii ,jumuiya na jamii zote zinaona mabadiliko haya ya tabianchi kila pembe ya dunia. Ndugu wote katika dunia hii wamesikika wakiongea athari mbaya zinaowagusa watu na hali ya nchi.

Na athari hizi zinajitokeza katika maeneo mbalimbali na hasa kwa wale wanyonge wanao dhulumiwa haki, watu masikini. Inapojitokeza matatizo au maafa katika maeneo ya wale wanaosababisha, ndipo huonekana dharura ya haraka katika haja ya kuwa na mabadiliko katika utendaji.

Tamko hili lasema, mabadiliko ya tabianchi ni mojawapo ya kikwazo cha maendeleo na huendeleza umasikini kwani matukio ya hali ya hewa yanasababisha njaa, maafa, kuyumba kwa uchumi, kulazimisha watu kuhama na kuzuia maendeleao endelevu.

Kipeo cha tabianchi kinahusu binadamu wote katika sayari hii ya dunia, Na hivyo inakuwa ni wajibu wa binadamu wote, kutathimini na kupata ufumbuzi wa haraka . Pamoja na hayo viongozi wa muungano wa madhehebu wanasema wako pamoja kutoa mchango wa kupunguza maafa yanayojitokeza, kama vile, kupunguza hewa ya ukaa ,kutoa elimu juu ya mabadiliko ya hali ya hewa, vilevile kuzuia matumizi mabaya ya mafuta.

Kwa Imani zao za kiroho na katika matumaini endelevu, watajitahidi ,kuchochea dhamiri binafsi na kuwatia moyo wenzao wote katika shughuli za kitume na jumuiya zote kufikiria hatua hizo kwa haraka.

Vilevile wanasema wanao uhakika kwamba suala linalohusu Tabianchi kamwe haliwezi kufanyika katika nchi moja , bali kwa ushirikiano wa Jumuiya zote za mataifa ,na hasa misingi ya kuaminiana, haki, na usawa, tahadhari, kurithisha kizazi na majukumu ya pamoja.

Wanatoa wito na kuhamasisha nchi tajiri kusaidia nchi zilizo masikini, ili nchi zote duniani na hasa katika nchi zinazopiga hatua za maendeleo kama vile mataifa yaliyoko Kusini mwa Jangwa la sahara ,wajitoe kwa ukarimu kusaidia ili nchi hizo zipate nguvu katika ufundi na teknolojia

Vilevile Wanawatia moyo viongozi wakuu wa mataifa , mawaziri wakuu kutoa hadi za kuchangia mifuko ya vyombo vina shughulikia na kupambana na uharibifu wa tabianchi, bila kusahau kwamba viongozi hao wakubaliane kuweka mikakati ya kuzuia ongezeko la joto la dunia lisizidi nyuzijoto 2.
All the contents on this site are copyrighted ©.