Jumapili 21Septemba yalifanyika maandamano makubwa katikati ya jiji la New York, Marekani,
yakiwa na lengo la kupaza sauti juu ya madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon alishiriki maandamano hayo akijumuika na wananchi
wote wakiwemo viongozi mashuhuri , na wanasiasa .
Taarifa kutoka Radio ya
Umoja wa Mataifa inasema kuwa Bwana Ban Ki Moon alisema hakuna kinachotegemewa
kufanyika zaidi ya mpango wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na zaidi ya kuchukua
hatua ambazo tayari zimeisha bainishwa. Alisitiza hakuna sayari nyingine ya dunia
ya binadamu kukimbilia na hivyo ni lazima kushirikiana na kuchukua hatua stahili.
Athari
za mabadiliko ya tabianchi ni pamoja na kuongezeka kwa kiwango cha maji ya bahari,
majanga ya asili na ongezeko la kiwango cha joto.
Maandamano ya jumapili yamefanyika
siku mbili tu kabla ya mkutano wa Katibu Mkuu kuhusu tabianchi kwenye makao makuu
ya Umoja wa Mataifa.
Mkutano huo utawaleta pamoja zaidi ya viongozi wa nchi
120, ili kuweka msukumo wa kufikia mkataba wa kimataifa kuhusu mbinu za kukabiliana
na mabadiliko ya tabianchi. Inatarajiwa kuwa mkataba huo utafikiwa mjini Paris, Ufaransa
hapo mwakani.
Idadi kubwa ya watu kukosa chakula haikubaliki:Vichi De
Marchi RipotI kuhusu wasiwasi wa ukosefu wa chakula duniani iliyowakilishwa
hivi karibuni mjini Roma inaonyesha ukweli wa vitu viwili , kwanza kupungua kwa watu
milioni 200 katika miaka 20 , na vilevile ukosefu wa chakula wa watu zaidi ya milioni
800.
Idadi hii hakubaliki alisema Bwana Vichi De Marchi mwakilishi wa Italia
katika idara ya Mpango na chakula wa Dunia ,alisema iwapo wenye njaa hasa katika
sehemu za Kusini mwa Afrika na Asia , inabidi siasa kuingilia kati.
Nchi ambazo
zimeweza kupambana na tatizo la njaa, ndizo zimekuwa mstari wa mbele kuchagua njia
ya kisiasa ili kutoa kipaumbele kukabiliana na tatizo hili, aliongeza Bwana Vichi.
Vilevile
waziri wa siasa katia masuala ya kilimo, chakula na misitu Bi Martina Maurizio aliongezea
kwamba katika mpango huo iwapo umoja wa Ulaya unataka ushindi juu ya changamoto hii
inapaswa iwe na ujasiri. Hata hivyo Italia inajitahidi kufanya kila njia ikitumia
matukio kama ya Expo ya Milan, kama njia mojawapo ya kutafuta mwafaka kamili .
Wito
wa Waziri Martina unasema,pamoja na kusubiri wanasiasa kutekeleza wajibu wao, kila
mwananchi anaweza kutoa mchango wake mdogo kama ule wa kuwa na umakini katika matumizi
mabaya ,au uharibifu wa vyakula, jambo ambalo kwa nchi zilizoendela limekuwa tatizo
sugu.
Akiongeza Mkufunzi wa siasa-kilimo na mwanzilishi wa (Last Minute Market)
chombo kinachohusu namna ya kuokoa vyakula alisema kwamba; inasaidia nini kuongeza
uzalishaji wa chakula asilimia 70% iwapo robo tatu ya chakula kinatumika hovyo? Aliwataka
watu wote watafakari.