2014-09-22 11:55:54

Ujumbe wa Papa katika Mkutano wa kimataifa juuu ya Injili ya Furaha


(Vatican Radio) Katika kikao cha Kimataifa kilichofanyika katika ukumbi wa Paulo wa VI Vatican kuhusu mpango wa kichungaji juu ya Injili ya furaha "Evangelii Gaudium"; Papa Francisko aliwaambia waliodhuria mkutano huo kwamba, wao ni wachungaji wa kanisa lote , na wameujumuika li kutafuta mbinu za pamoja za kutekeleza mipango wa kichungaji juu ya Injili ya Furaha. Ni suala la Msingi katika utume wa Kanisa , na ni wajibu wao kutoa majibu ya ujumbe huo.
Papa alisema kwamba anakumbuka jambo moja kichwani mwake juu ya Injili ya Mtakatifu Matayo “ alipouona umati ,alishikwa huruma kwa sababu walikuwa wamechoka na kama kondoo wasiokuwa na mchungaji” ( Mt 9,36)
Nyakati zetu hizi ni watu wangapi walioko pembeni, wamechoka, na wanasubiri Kanisa, wanasubiri sisi! Ni jinsi gani ya kuwafikia, ni namna gani ya kushiriki nao uzoefu wa imani , na upendo wa Mungu, na kukutana na Yesu. Huu ndiyo wajibu wa Jumuiya zetu na uchungaji wetu, Baba Mtakatifu alielezea.
Na kwamba, wanayo kazi ya kutafakari juu hali ya nyakati hizi (Evangelii Gaudium, 51)lakini yeye anaalika kanisa zima kupokea ishara za nyakati , ambazo Bwana anatoa bila kupumzika. Ni ishara ngapi zilizoko katika Jumuiya , kuna uwezekano upi ambao Bwana anaweka mbele ili kujua uwepo wake katika dunia ya leo! Papa alibainisha kwamba; matukio mabaya katika nyakati hizi ndiyo yanayofanya kelele zaidi , na kufanya ishara za matumaini yanayotia nguvu na ujasiri zifunikwe . Ishara hizi zinapaswa zitambuliwe kwa kupitia mwanga wa Injili, maana huu ni wakati mwafaka (2 Kor 6,2)
Kipindi cha kujibidisha kikamilifu, ndiyo kitovu msingi cha kutenda kwaajili ya kukuza ufalme wa Mungu, umasikini na upweke unaokena katika ulimwengu wa leo, watu wangapi wanazi kuishi katika matatizo na wanaomba kanisa liwasaidie , Kanisa liwe karibu nao, kwa njia ya mshikamano na huruma ya Bwana. Hii ni kazi kubwa na hasa wale waliokabidhiwa uchungaji, kama Maaskofu wa Jimbo, Maparoko katika Parokia , Shemasi katika kazi ya upendo, Makatekista katika wajibu waa kushuhudia imani, kwa ujumla watu wote walioitwa kutambua na kusoma ishara za nyakati na kutoa jibu la hekima na ukarimu, alitoa mwongozo Baba Mtakatifu.
Mbele ya mahitaji mengi ya watu hawa wanaoteseka kwasababu ya maombi mengi, wanaume na wanawake, wale walioitwa kutenda kazi hiyo wanaogopa na kuona hatari na hivyo kujifungia wao wenyewe katika mtazamo wa ofu una kujihami, na ndipo majaribu yanajitokeza kukimbilia katika sheria, kama walivyokuwa wakifanya waandishi, Mafarisayo na wanasheria wakati wa Yesu.
Papa anawaonya ya kuwa,watakuwa na kila kitu sawa, na kila kitu kimepangwa, lakini ikumbukwe kuwa waamini , wakristo wanazidi kutafuta na wataendelea kuwa na njaa na kiu ya Mungu.
Papa anabainsha kwamba amesema mara nyingi kwamba Kanisa ni kama Hospitali iliyoko kambini: watu wengi walio umia wanao hitaji wasogelewe na sisi, wakiomba sisi kile ambacho walikuwa wakimuomba Yesu, ukaribu na uwepo : Lakini kwa tabia hii yakuwa watumishi kuwa walimu wa Sheria , na mafarisayo , kamwe hatutaweza kuwapatia ushuhuda wa ukaribu.
Pia Baba Mtakatifu aliongeza mfano mwingine wa tafakari juu ya Bwana na shamba la mizabibu akiwa anahitaji wakafanyakazi, alitoka nyumbani masaa tofauti kwa siku na kuwaita katika shamba lake (Mt 20,1-16)
Yeye hakutoka mara moja tu , katika Injili wanasema Yesu alitoka karibu mara tano , alfajiri, saa tatu, saa sita, saa tisa na saa kumi na moja za jioni. Aliongeza kuwa: hata sisi tunao muda inawezekana akaja kwetu! Kulikuwa na mahitaji ya wafanyakazi na ndiyo maana kutwa nzima akashinda anazunguka sehemu zote kuwatafuta wafanyakazi.
Ukifikiria watu hawa ambao kwa muda huo hakuna mtu aliyewaita , je walijisikiaje, kwasababu mwisho wasiku hakuwa na kitu chochote cha kupeleka nyumbani kwaajili ya watoto wao. Hivyo ni wajibu gani wachungaji na wahudumu walio nao katika shughuli za kichungaji , Papa alishauri ni vema kutafuta sehemu hii ya injili ikawa mfano na kuitakari kwasababau ya uchungaji .Inabidi kuwafikiria na kuwafikia wanyonge , wote na kuwapatia kitulizo wajisikie na kuwa katika shamba la Bwana, hata kama ni saa moja tu. Alisema Papa
Baba Mtakakatifu aliongeza ni jinsi gani anavyojua majitoleo yao katika shughuli zao za kiuchungaji lakini kitu cha msinhi ni kuonyesha ushuhuda , maana ushuhuda ndiyo mwanzo wa unjilishaji ambao unamfikia mtu ndani ya moyo na kuleta mabadiliko, maneno matupu matendo hayahitajiki , ushuhuda zaidi unaoleta maana zaidi ya maneno.
Alimalizia kwa kuwashukuru kwa utume wao na kuwabariki, akiwaomba wasisahau kusali kwa ajili yake, kwasababu alisema kuwa anapaswa kuongea sana lakini zaidi anapaswa atoe naye ushuhuda wa kikristo.








All the contents on this site are copyrighted ©.