2014-09-20 15:55:26

Papa anakwenda Albania kupeleka ujumbe wa amani na mshikamano


Jumapili hii 21 Septemba 2014, Baba Mtakatifu Francisco, anafanya ziara ya Kitume katika mji wa Tirana Albania. Hii ni ziara ya Pili kwa Kiongozi wa Kanisa la Ulimwengu kutembelea Albania nchi yenye historia ya tangu mwanzo wa Kanisa, ambako Mtume Paulo alipatembelea. Ziara ya kwanza ilifanywa na Mtakatifu Yohane Paulo 11 hapo tarehe 25 April, 1993, ikiwa imepita miaka miwili baada ya kuagushwa kwa utawala wa kidikteta wa kikomunisti. Papa aliweza kutembelea Albania baada ya kuanzishwa kwa mahusiano ya kidiplomasia kati ya jimbo la Papa na Jamhuri ya Albania.

Katika ziara ya Jumapili hii, ambayo ni ziara ya siku moja, nia kuu ni kupeleka ujumbe wa amani na mshikamano Albania. Papa akiwa huko atakutana na viongozi wa utawala wa Kiserikali na wanadiplomasia, kuongoza Ibada ya Misa, na kutembelea Kanisa Kuu la Scutari , ambalo wakati a utawala wa kikomunisti liligeuzwa kuwa eneo la michezo mwaka 1967, na lilitabarukiwa upya muda mfupi kabla ya ziara ya Papa Yohane Paulo 11. Pia atakutana na viongozi mbalimbali wa kidini, na kuongoza Ibada ya Msifu ya jioni na atatembelea kituo cha watoto cha Betania.

Papa atarejea Vatican Jumapili hiyohiyo majira ya jioni.
All the contents on this site are copyrighted ©.