2014-09-20 15:26:00

Papa- ufufuko ni mabadiliko ya miili yetu.


Ijumaa 19 Septemba katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta Vatican, Papa aliadhimisha ibada ya Misa ambamo katika homilia yake,alilenga zaidi juu ya Neno la Mungu, kutoka barua ya kwanza ya Mtakatifu Paulo kwa Wakorinto, ambamo Wakristo wanaonekana kuwa na matatizio ya kuamini mabadiliko ya miili yao baada ya kifo.

Alisema kwamba Mtume wa watu alikwenda kuwaeleza Wakristo Wakorinto, wale ambao waliamini kwamba Kristu amefufuka, lakini walikosa mwanga zaidi kwamba hata na wao watafufuka, wao walifikiri kwa namna nyingine, ya kwamba wafu wamekwisha hukumiwa.

Hata hivyo siku ya kwanza ya Juma ya ufufuko wa Yesu , hata Mtakatifu Petro alikimbia kwenda kaburini akifikiri kwamba mwili wa Bwana umeibiwa vilevile hata Maria wa Magdala. Hawakukumbuka ufufuko wa kweli, walishindwa kuelewa njia ya kutoka katika kifo kuufikia uzima ni kwa njia ya ufufuko.

Waliupokea ufufuko wa Yesu kwa sababu walimuona Yesu. Papa aliongeza, hata hivyo ufufuko wa Wakristo haukuwa hivyo maana hata Mtakatifu Paulo alipokwenda Atene na kuanza kuhubiri juu ya ufufuko wa Kristo watu walilamika, mpaka wagiriki wenye hekima, na Wataalimungu waliogopa.

Ufufuko wa wakristo ni kashfa, ni vigumu kuutambua, na ndiyo maana Paulo aliwaza hivi; “kama Kristo amefufuka , inawezekanaje kati yenu kusema hakuna ufufuko katika wafu?”

Anabainisha Papa, kuna ugumu wa kupokea mabadiliko, ugumu ambao kazi ya Roho Mtakatifu tuliyempokea kwa njia ya ubatizo anao uwezo wa kubadili mpaka mwisho , hadi katika ufufuko.

Alitoa mfano ,tunapoongea juu ya hilo , “tunasema mimi ninataka kwenda mbinguni, sitaki kwenda ahera, natunasimama pale pale, hakuna anayesema ,mimi nitafufuka kama Yesu, hakuna, kwa hiyo hata sisi ni vigumu kutambua jambo hilo.

Ni rahisi kwa wanaosadiki kuwa ulimwengu wote kuna miungu wengi, sababu yake wanaamini kuwa kuna uwezekano wa kubadilika, hata hivyo neno “kubadilika ”ni neno ambalo Mtakatifu Paulo alilitumia ya kwamba tutabadilishwa. Miili yetu itabadilishwa, alitoa mfano wa jinsi watu hupatwa na hofu wanapokuwa katika tiba ya kupasuliwa hospitalini, wana woga wa kutolewa kitu fulani ndani ya mwili wao ,au kuwekewa kitu fulani… na hivyo kusababisha mabadiliko, kwa kusema hivyo hata katika ufufuko wote tutabadilishwa.

Hali hiyo ndiyo inayotusubiri siku zijazo , na ndiyo inayotufanya tuwe wagumu: ugumu hasa wa kubadilishwa miiili yetu. Hata ugumu wa kuwa na uthibitisho wa Mkristo. Papa alitoa mfano mwingine ya kwamba inawezekana hatuogopi ufunuo wa mabaya, au wale wanaompinga Kristu ambaye atarudi tena, hatuogopi. Labda hatuna uoga wa sauti ya malaika, au sauti ya baragumu:kwakuwa itakuwa ni ushindi wa Bwana.

Bali tunao woga wa ufufuko wafu. Wote tutabadilishwa, na ndiyo utakuwa mwisho wa safari yetu ya ukristo, yaani ile ya kubadilishwa.

Lakini kishawishi hiki cha kutokuamini ufufuo katika wafu, hata mwanzo kabisa wa Kanisa ilikuwepo,hata Mtakatifu Paulo alipoongeea kwa watu Wathesalonike, katika barua yake aliwatuliza na kuwatia moyo wawe na matumaini, maana mwisho tutakuwa naye.

Alimazia kwa kusema kwamba uthibitisho wa Mkristo na njia yake , ni safari ambayo yupo Bwana , kama wale mitume wawili waliotembea na Bwana na mwisho wakabaki naye jioni, tunaitwa maisha yetu yote kuishi na Bwana , na mwisho tutakaposikia sauti ya malaika baada ya mlio wa baragumu tutabaki naye.
All the contents on this site are copyrighted ©.