2014-09-19 14:46:32

Yesu anawatia moyo wadhambi kujitambua


(Vatican Radio) Ni mafundisho ya baba Matakatifu aliyoyatamka Alhamis 18 Septemba katika mahubiri yake ndani ya kanisa dogo la Mtakatifu Marta Vatican.
Papa alisema Liturgia ya neno,leo inatufikisha katika tukio la mwanamke anaye muosha Yesu miguu yake kwa machozi , na kumkausha kwa nywele zake, na kumpaka manukato.

Yesu alikaribishwa kwenye nyumba ya mfarisayo mmoja, mwenye ujuzi na hata elimu, ambaye alitaka kumsikiliza. Mafunzo hayo ilikuwa ni kutaka kujua zaidi, japokuwa anamhukumu rohoni mwake yule mwenye dhambi, na kuhukumu pia Yesu mwenyewe akisema “kama angekuwa ni nabii angejua ni nani mwanamke anayemgusa”

Papa aliongeza,Mfarisayo hakuwa mbaya , bali hakufahamu kitendo kile alichotenda mwanamke. Alishindwa kuelewa ishara msingi za watu, labda mtu huyo alikuwa amesahau namna gani wanavyo bembeleza watoto , au kumfariji mzee.

Katika mafunzo yake, katika fikira zake, na katika maisha ya utawala wake, labda alikuwa ni mshauri wa wafarisayo, alikuwa amesahabu ishara msingi za maisha, ambazo kila mmoja wetu mara anapozaliwa alizipokea kutoka kwa wazazi wake.

Yesu alimkaripia mfarisayo, aliongeza Papa, lakini kwa unyenyekevu, huruma, subira, na upendo wake wa kutaka kuwaokoa wote, unamfanya Yesu awaelezee juu ya ishara ya mwanamke kufanya kitendo hicho ya kwamba; hakumfanyia yeye.

Lakini pamoja na wengi kutoa kashifa na masengenyo kwa mwanamke huyo, wanasikia “dhambi zako zimeondolewa, nenda kwa amani , imani yako imekuokoa”
Neno Wokovu, Papa alisema, imani yako imekuokoa, ni neno alilomweleza mwanamke mwenye dhambi, ni kwa sababu alijutia dhambi zake, aliungama dhambi zake, na kusema yeye ni mwenye dhambi.
Hakuwaeleza wale ambao hawakuwa wabaya, wao waliamini hawana dhambi, wenye dhambi walikuwa ni wengine, watoza ushuru na makahaba hawa ndiyo walikuwa wanahesabiwa wenye dhambi.
Lakini Yesu alisema umeokolewa wewe,ni maneno anayoyatoa kwa yule tu anayejua kufungua moyo wake na kijitambua mwenye dhambi. Wokovu wa roho ni kwa wale tu wanaojua kujifunua kweli na kutambua dhambi zao.
Watu wenye dhambi wanayo nafasi mwafaka ya kukutana na Yesu alibainisha Papa na kutoa mfano, katika jambo hili unaweza kufikiri ni uzushi lakini hata Mtakatifu Paulo anajivunia kwa mambo mawili ya dhambi zake na ya Kristo mfufuka aliye mwokoa, alidhihilisha Papa.
Kwa namna hiyo kujitambua dhambi zetu wenyewe, kutambua udhaifu wetu, ni kujiambua sisi wenyewe, kutambua kile tulicho na uwezo nacho. pia kile tusichojua kufanya, ni dhahiri kuwa mlango unafungua njia katika mbeleko ya Yesu, msamaha wa Yesu, na Neno la Yesu asemaye “Nenda kwa amani, imani yako imekuokoa, kwakuwa umekuwa na ujasiri wa kufungua moyo wako kwa yule tu ambaye anaweza kukuokoa.
Yesu aliwambia wanafiki, makahaba na watoza ushuru watawatangulia mbele katika ufalme wa mbingu…”Ni neno lenye uzito” alimalizia Papa, kwani wengi wanaojisikia wadhambi, wanafungua mioyo yao katika sakramenti ya kitubio, kuungama dhambi na kukutana na Yesu ambaye amemwaga damu kwa ajili ya wote.
All the contents on this site are copyrighted ©.