(Vatican Radio)Jumatano baada ya katekesi yake, Papa pia alizungumzia umuhimu wa
ziara yake ya Kitume Albania Jumapili 21Septemba 2014 akisema kwamba; kwa msaada
wa Mungu, ataweza kwenda Albania, kutembelea nchi hiyo sababu ya mateso makubwa waliyoyapata
kutokana na utawala wa kidikiteta wa kikomunisti, na sasa hali ya amani imeanza kujionyesha
katika ya madhehebu mbalimbali ya kidini.
Na aliwatumia salamu watu wa Albania
akiwashukuru kwa maandalizi wanayo fanya kwa ajilli ya kumpokea. Na mwisho aliwaomba
watu wote, wamsindikize kwa sala katika ziara hii. kuomba msaada wa Mama Maria wa
shauri jema.
Katika matatizo yaliyowakumba watu wa huko Albania kwenye kipindi
cha utawala wa kikomusiti Sista Maria Lucia wa Shirika la Mabinti Wadogo wa Yesu,
anayefanya utume Tirana alipata ya kuongea na mwandishi wa habari wa Radio Vatican
akisema inabidi kukumbuka kwamba Kanisa wakiwemo Wakatoliki Albania walipata masumbuko
makubwa sana kwa kipindi cha utawala wa Enciver Hoxha.
Kwa kipindi cha miaka
50 wamekuwa kimya na Woga mkubwa, licha ya udikteita, utawala huo nchini Albania
kulianguka miaka 23 iliyopita, na hivyo sehemu kubwa ya Mtaguso wa Pili wa Vatican
unakosa katika kanisa katoliki la Albania.
La kushangaza baada ya kuanguka
kwa utawala huo mwamko mzuri umekuwepo kwa watu wote wa Albania wakiwa wameungana
na waislam,na Ortodosi katoliki . Tangu mwanzo Kanisa la Albania limekuwa na uhusiano
mzuri na wamisionari waliofika kwa mara ya kwanza kutoka nje, ni uhusiano ambao mpaka
leo bado unaendelea ,pia miito kwa upande wa mapadre mahalia nao umeanza kuchanua,
na zaidi kwa upande wa watawa wa kike na kiume, hii hakika ni ishara ya matumaini.
Pia
sista alito ushuhuda wake kuhusu maelewano kati ya madhebu mbalimbali ya dini, kutokana
na uzoefu wake alioufanya nchi ya Kosovo ambayo pia ilikuwa na hali kama hali ya
nchi ya Albania, ya kwamba mwanzo walikuwa wakiishi katika vijiji vay pembeni na wakristo
walikuwa wachache, zaidi walikuwa waislamu lakini pamoja na kuishi mchanayiko wa
madhebu tofauti waliishi vizuri.
Katika mazingira ya mji mkuu Tirana anabainisha
Sista kuna ushirikiano kati ya madhehebu yote ya kidini, waislam na wakatoliki na
wanashiriki katika maisha ya furaha, kwa kupeana zawadi wakati wa sikukuu mbalimbali,
wanapongezana na kusaidiana wakati wa shida.
Sista anamalizia akisema kwamba
kitenda cha kufika Papa Fransisco katika nchi ya Albania ni muhimu sana , kwa kuwatia
moyo wa kuendeleza ushirikiano na maelewano kati ya madhehebu, na zadi ya hayo katika
harakati zinazofanyika kumpokea Papa anayo furaha kubwa kuona kuwa vyombo vya habari
nchini Albania vimetoa kipaumbele juu ya ujio wa Papa Francisco.