Makatekista -Injilisheni kuanzia ndani ya familia zenu
Semina ya makatekista wa Jimbo la Roma imemalizika Jumanne 16 Septemba, katika Jimbo
la Roma kwa ajili ya kuwaandaa Makatekista katika ufundishaji wa elimu ya dini Parokiani,
juhudi mpya za kitume zinazo anza hivi karibuni baada ya likizo ya miezi mitatu ya
kiangazi.
Ni utume wa kanisa kwa watoto na vijana kupokea mafundisho msingi
ya kanisa wakiwa wadogo na kuendelea. Katika semina hiyo, wazo kuu limekuwa ni kuangalia
upya mbinu za kuinjilisha vijana, kwa kuanza katika familia zao. Makatekista wameombwa
kuwa na imani kuu kwa Mungu inayochotwa kutoka Injili, ili iwape mwanga wa kuachanganua
maisha yao.
Pia makatekista waliombwa kuwa na elimu zaidi, kwani itawasadia
katika kukabiliana na vijana watakaokutana nao katika parokia na kuweza kuwasaidia
katika changamoto zao na kuwapa uhusiano mzuri na matumaini.
Na katika kufunga
semina hiyo ya makatekista, Kardinali Agustino Vallini Decano wa Dekania ya Roma
alisema, ili kuweza kugusa moyo wa kijana wa leo, inahitaji upendo mkuu kwani vijana
wa siku hizi wako tofauti kulinganisha na kizazi kilichopita katika hali zote, mabadiliko
yanayotokana na changamoto wanazokutana nazo , hivyo hakuna maana ya kupunguza mafunzo
ya katekisimu wanapofika kwenye mafunzo hayo , maana mafunzo haya ndiyo msingi, ndiyo
chemichemi .
Inahitaji kuwajibika kwani ni utume mkubwa na parokia ndiyo sehemu
muhimu ya kupokea habari njema na kupeleka habari njema kwa vijana na kwa familia
zao , ambazo kwa nyakati hizi imani inaelekea kuyumbayumba.
Naye Pia Mkurugenzi
wa ofisi ya Katekesi Jimbo la Roma Padre Andrea Lonardo, aliwakumbusha maneno ya
Papa Fransisko anavyosistiza juu ya parokia, kwani inapaswa kuwa karibu na watu,
na watu vilevile waonekane katika parokia, isiwe tabia ya watu kuonekana wakati wa
misiba, ubatizo au kupokea kumunyo ya kwanza.
Vilevile alisema kwamba, Papa
anapenda kuona Parokia zinapaswa kufunguliwa kupokea watu wote bila mipaka. Na Parokia
zinapaswa zitoke nje kuangalia watu wanoteseka na matatizo mbalimbali ya kimwili na
kiroho, sehemu zenye matatizo ya elimu, matatizo ya wagonjwa , wasio kuwa na mtu wa
kuwaangalia , walemavu katika hali zote.
Kuna matatizo ya vijana wengi wanapomaliza
kupokea kumunio Takatifu ya kwanza wanapotea, na hivyo ni famila ambazo inabidi zigundue
kwa upya uzuri wa kuwa na imani kwa Mungu,na pia familia zinapswa zionyeshe mifano
ya imani kwa Mungu kwa watoto wao.Kwani katika ujana mambo ya utoro kanisani hayakosekani
na hivyo ni muhimu kwa wazazi kuwasindikiza watoto wao kaika njia za makuzi ya vijana
hasa kutembea ndani ya Kanisa.