2014-09-16 08:07:07

Caritas yafanya mpango wa dharura kwa ajili ya mafuriko India


Shirika la caritasi hivi karibuni lilitoa habari kuhusu kuomba msaada kwaajili ya watu zaidi ya milion 3,5 nchini India baada ya mafuriko mabaya yalioyoikumba baadhi maeneo mbalimbali ya nchi.

Wasiwasi mkubwa ni juu ya watu walio rundikana bila kuwa nyumba na msaada kwani maeneo mengi ya ardhi na nyumba vilipelekwa na mafuriko hayo, itachukua muda kuweza kurudia hali na kukarabati maeneo hayo.

Shirika hili linatoa ripoti kwamba pamoja na juhudi hizo za kuweza kuwasaifda watu walikumbwa na mafuriko hayo , linahitaji kukusanya kiasi cha euro 768 elfu kwaajili ya kuwasidia milioni ya watu ambao wamepoteza nyumba na kila kitu, katika maji.

Linaongeza mpango huko wa dharura unakadiriwa kufanyika ndani ya miezi 8 ukiwa na mategemeo ya kuwasidia watu 47,000 wa maeneo mabambali ya nchi na hasa waliokumbwa na mafuriko hayo.

Mpango huo unategemea kujenha na kukarabati nyumba, kuweka nyumba za dharura kwaajili ya familia zisizo na mahali pa kukaa kwa muda mfupi, na kuboresha meeneo hasa kwaajili ya afya kwa ujumla.

Na zaidi ya hayo Caritas ina mpango wa kutafuta miundo mbinu ya teknolojia na kilimo, ikitaka kutoa hata vifaa , mbegu, na wanyama kwaajili ya maendeleo endelevu katika uchumi.

Hata hivyo pia inahitaji kuweka mpango wa kuweka akiba kwaajili ya dharuara ya mafuriko iwapo yanaweza kutokea tena.

Baraza la Maaskofu India laonba Msaada
Mwenyekiti wa Baraza la maaskofu India (CBCI) Kardinali Baselios Cleemis, ameomba watu wote zaidi ya wakatoliki million 16 India kuwa na ukarimu wa kujitoa kusaidia watu wa maeneo ya Jammu na Kashimir , maeneo ambayo yamekumbwa na mafuriko.

Katika wakaraka wake alielelezea wasiwasi mkubwa alio nao kuhusu watu ambao wamepoteza maisha yao, na wengine wengi kupoteza ardhi, nyumba zao kubomolewa na maji.

Inasemekana kwamba zaidi ya watu 200 walikufa , na ekari za ardi kupelekwa na mafuriko.
Barabara kuu ya mji zilifungwa kwa siku 9 kutokana barabara nyingi kubomoka au kupelekwa na maji, kiasi cha hata waziri Omar Abdallah, kuomba msaada wa dharura wa kuomba mashine za kupamp maji katika maeneo mengi ya makazi ya watu.

Timu za madaktari na wataalamu mbalimbali wakiwemo wataalumu wa magonjwa ya mlipuko , walipelekwa huko, na pia Tani 1000 za madawa zinahitajika kumpambana na magojwa ya tumbo kuhala na pia chakula.Bado katika maeneo ya Ramban na Banihal maelfu ya tani za maji zinahitajika kukidhi haja ya watu.

Zaidi ya mahema 80 yametayarishwa kwaajili ya watu wasiokuwana makao, pia juhudi za vikosi vya kuokoa vinaendelea na mpango wa kupeleka mahema mengine , vyakula , vifaa vya kujifunika nk , lakini pamoja na juhudi hizo watu ni wengi na vifaa hivyo haviwatoshi alisema Kardianali Baselios.Bado pia tatizo kubwa la njia za kimawasiliano na hivyo kuhitajika nguvu zaidi ya utengezaji wa barabara hili watu waweze kufikiwa msaada.

Aliongeza suala la ukosefu wa mahali pa kuishi ni kubwa kwa watu walio salia na mafuriko kwani zaidi ya nyumba 20,000 zilianguka na nyingine nyingi zinzahitaji kukarabatiwa.

SIku ya Kimataifa ya Ushirikiano wa Kisni mwa Sayari ya Dunia
Ijumaa 12Sept2014 ilikuwa ni siku ya Kimataifa ya Ushirikiano wa Kusini mwa Sayari ya Dunia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa , Ban Ki Moon alisema kuwa siku hiyo ya mwako huu inakuja wakati jamii ya kimataifa ikiwa kwenye kipindi cha mpito kuelekea ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015, ambayo inazingatia ufanisi wa pamoja na uendelevu wa mazingira.

Bwana Ban aliongeza, pamoja na kupiga hatua kubwa katika kufikia malengo ya maendeleo ya Milenia, (MDGs) hatua za maendeleo kwenye nchi za kusini mwa dunia bado haziwekwa sawa.Kwasababu umaskini uliokithiri, ueneaji wa kutokuwepo usawa, utapiamlo na kuwa hatarini kuathiriwa na majanga ya tabianchi na hewa bado vimeshamiri.

Kwa mujibu wa takwimu za mseto za Umoja wa Mataifa kuhusu umaskini, watu bilioni 2.2 bado wanaishi katika umaskini uliokithiri. Aliongeza kuwa watu wapatao bilioni 1.4 –wengi wakiwa kusini mwa sayari dunia- hawana umeme, huku watu milioni 900 wakiwa hawana maji safi na bilioni 2.6 hawana huduma tosha za usafi kwa ujumla.

Ban Ki moon alisema kuwa ushirikiano wa Kusini mwa Dunia unatoa fursa nyeti ya kuleta usawa katika ukuaji maendeleo katika ushirikiano wa kimataifa kuhusu maendeleo endelevu.

Mahitaji ya madini ya urani itumikayo katika vituo vya nishati kupanda: (IAEA)
Mahitaji ya madini ya urani, malighafi inayotumiwa kama nishati ya vituo vya nguvu za nyuklia duniani kote, itaendelea kupanda katika siku za karibuni, licha ya kushuka kwa bei za soko tangu ajali ya kituo cha umeme cha nyuklia cha Fukushima Daiichi nchini Japan Machi 2011, sambamba na mahitaji ya chini ya umeme kwa sababu ya mtikisiko wa uchumi duniani.

Haya ni miongoni mwa matokeo ya msingi ya riporti mahususi iliyotolewa 10Sept2014 na Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki pamoja na Kitengo cha nishati ya Nyuklia cha Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo, (OECD)Ripoti hiyo ijulikanyo kama Red Book, imeelezea kuongezeka kwa urani, utafutaji na pia uzalishaji .

Tangu kuchapishwa kwa ripoti ya mwaka wa 2012, asilimia saba ya raslimalia ya urani imetambuliwa na hivyo kuongeza karibu miaka 10 ya rasilimali zilopo. Inasemakana kwamba uzalishaji wa urani duniani kati ya mwaka 2010 na 2012 , umeongezeka japo ni kwa kisai kidogo kuliko kipindi cha miaka miwili ya awali.

Ubia mpya wazinduliwa kuokoa misitu ya dunia (UNEP,IUCN)
Hivi karibuni mwezi huu Sept2014 ulizinduliwa ubia mpya wa kuokoa misitu ya dunia katika ya Shirika la Mpango wa Mazingira (UNEP) na Muungano wa Kimataifa wa Kuhifadhi Maliasili (IUCN).

Juhudi za kupambana na mabadiliko ya tabianchi na kuboresha maisha kwa kulinda misitu zimepewa msukumo mpya ambapo uzinduzi huu mefanyika wiki chache Kabla ya mkutano wa kilele wa hali ya hewa iliyoandaliwa na Katibu Mkuu Ban Ki-moon katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York ambayo itafanyika tarehe 23 Septemba.

Ushirikiano huo unalenga kurejesha misitu iliyoharibiwa kwa kuhakikisha kuna tena ekari milioni 150 za misitu ifikapo mwaka 2020. Ushirikiano huo utaleta pamoja mikakati miwili muhimu ya kimataifa inayoendelea ya kuokoa ardhi iliyomomonyoka, ambayo ni Mpango wa pamoja wa Umoja wa Mataifa wa Kupunguza Uchafuzi utokanao na Uharibifu wa Misitu, UN-REDD na Ubia wa Kimataifa kuhusu Kuokoa kwa Ardhi ya Misitu pamoja na kusaidia ufumbuzi wa nishati safi.

Serikali ya Ujerumani hivi ilitoa dola bilioni 1 za kimarekani kwaajili mfuko wa mpango wa kupamabana na mabadiliko ya tabianchi ikiwa ni mchang wa kwanza katika mfuko huo, na michango mingine inategemewa mwezi novemba mwaka huu wakati wachangiaji watatangaza michango yao kwaajili ya kuimarisha mfuko huo.
All the contents on this site are copyrighted ©.