2014-09-16 14:53:43

Askofu Mkuu Mamberti atembelea Georgia


Katibu kwa Mahusiano na Nchi zingine Vatican,Askofu Mkuu Domenique Mamberti, anatembelea Georgia. Ziara aliyoianza siku ya Jumamosi na anakamilika Jumanne hii, Septemba 16, 2014.

Tarifa inaleza Jumatatu, Septemba 15 alikutana na Waziri Maria Panjikidze wa Mambo ya Nchi za Nje Georgia, ambamo walijadili wigo mpana wa mahusiano baina ya Vatican na Georgia, nchi na kusisitiza umuhimu wa ziara hii katika suala la Kuimarisha uhusiano wa kirafiki kati ya mbili mataifa.

Na hivyo pande zote zilisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa karibu katika nyanja ya kitamaduni, kielimu na kibinadamu. Askofu Mkuu Dominique Mamberti alithibitisha utayari wa Kiti Kitakatifu, kuendelea kusaidia Georgia katika siku zijazo.
Pia uwakilishi wa Kiti Kitakatifu uliweza kupewa taarifa mpya za maboresho yaliyofanya na serikali katika sera zake za mageuzi katika uwanja wa ulinzi wa haki za binadamu. Askofu Mkuu Dominique Mamberti alirudia kutoa misistizo katika kudumisha heshima kwa uhuru Georgia, uadilifu na sera mashirika yasiyo tambuliwa bado kiserikali.

Pia Askofu Mkuu Dominique Mamberti alikutana na Rais wa Georgia, Mheshimiwa Giorgi Margvelashvili, na Waziri Mkuu, Mr Irakli Garibashvili na Spika wa Bunge, Mheshimiwa davit Usupashvili.

Aidha kati ya matukio ya kukumbukwa katika ziara hii , ni Askofu Mkuu Mamberti , kuweka shada la maua katika mnara wa Makumbusho ya watu waliofariki wakati wa machafuko ya kuleta Uhuru Georgia. Na ameifunga ziara yake kwa kutembelea Khurvaleti. Jumapili Tarehe 14 Septemba, Ndani ya mfumo wa ziara hiyo, Askofu Mkuu Dominique Mamberti alipokelewa na Mtakatifu na Mwenyeheri Catholicos- Patriaki wa Georgia yote.
All the contents on this site are copyrighted ©.