2014-09-13 15:58:37

Ziara ya Papa Redipuglia asema -Vita ni wazimu.


Mapema Jumamosi hii, Baba Mtakatifu Francisko aliongoza Ibada ya Misa katika makaburi ya kijeshi ya Redipuglia, Friuli Venezia Italia. Katika eneo hilo kuna makaburi ya watu waliofariki katika Vita Kuu ya kwanza ya Dunia. Papa amekuwa katika eneo hilo kwa nia ya kuziombea Roho za Marehemu waliofariki katika vita hivyo , ambavyo mwaka huu imetimia miaka mia tangu vilipoanzishwa. Ziara ya Papa Francisco inavunja ukimya wa miaka 22 , kwa eneo hilo kutembelewa na Papa ambako mara ya mwisho lilitembelewa na Mtakatifu Papa Yohane Paulo 11, 3 Mei 1992.

Akiongoza Ibada hiyo, katika homilia yake, alitafakari mazingira mazima ya eneo hilo, akisema baada ya kutembea na kuona mazingira mazuri ya kuvutia, watu wakifanya kazi wake kwa waume na familia zao , watoto wakicheza mitaani na wazee katika ndoto zao", sasa ninajikuta katika eneo hili waliko lala maelfu kwa maelfu ya watu, ninachoweza kusema ni tu kwamba "vita ni wazimu. "

Aliendelea kusema "pale Mungu anapoongeza viumbe wake, sisi binadamu tunatakiwa kushirikiana nae katika kazi zake za uumbaji na si kutengeneza mipango ya vita vya kuharibu. Ni unyama wa namna gani huu kuharibu hata kilichoumbwa kwa ustadi na Mungu mwenyewe, uwepo wa binadamu. Vita huharibu kila kitu hata dhamana kati ya ndugu. Vita ni wendawazimu, maendeleo yake ni mipango wa uharibifu. Ni njia ya uharibifu mtupu.

Papa aliendelea kuonya na kutaja sababu kuu za uwepo wa vita kuwa ni uchoyo, kutovumilia, tamaa ya mamlaka , ushabaki ... hizi ni sababu zinazo shinikiza mtu kutoa maamzi ya vita, hizo ni sababu ambazo mara hujenga itikadiza vita ; lakini kwanza kabla nyuma yake kuna shauku, kuna msukumo potofu. Itikadi huhesabika kama jambo la haki, na pale ambapo hakuna itikadi , kuna kishindo cha jibu lililofinyangwa, jibu kama lile la Kaini, ya Kaka yangu yananihusu nini ? Kwani mimi mlinzi wa ndugu yangu? (Mwa 4.9) ". Vita haitazami usoni, huathiri watu wote, wazee, watoto, wanawake, wanaume , akina baba na akima mama ...Lakini wanaoandaa vita hivyo ndani mwao husema, "sijali?".

Homilia ya Papa iliendelea kuzungumzia wanaopuuzia uharibifu wa vita, akisema yeye yuko wa tofauti nao,yuko mbali na wote wale wanaosema sijali, yeye anajali wingi wa watu hao waliopumzika katika makaburi hayo kwa sababu za uharibifu wa binadamu. Watu hao wote, waliopumzika hapo, walikuwa miradi yao, wao alikuwa na ndoto zao, walikuwa na maisha yao ... lakini maisha yao yalikatishwa na kusambatishwa kama vile hayakuwa na maana. kwa sababu mtu mwenzao alisema sijali.

Hata leo, baada ya kushindwa kwa vita vingine vya pili vya dunia, labda tunaweza kuzungumzia vita ya tatu iliyogawanyika katika vipande vipande, vya uhalifu, mauaji, uharibifu ...ambamo ukurasa wa kwanza wa magazeti juu ya vita hivi unaweza kuwa na jina, kwangu mimi sijali, kama alivyosema Kaini " kwani Mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?".

Papa alionya tabia hii ni kinyume kabisa na kile Yesu anachoomba katika Injili. Yeye alionekana kuwa mdogo kai ya ndugu zake lakini ni yeye aliye Mfalme, Mwamuzi wa dunia, Yeye alishikwa na njaa, kiu, ukiwa, mgeni, mgonjwa na mfungwa ...Yeye anayewahudumia ndugu zake, huipata furaha ya Bwana; wale ambao hawana, ambao pamoja na upungufu wanaendelea kusema, mimi sijali, basi wote hao hubaki nje ya furaha hiyo.
All the contents on this site are copyrighted ©.