2014-09-13 09:12:44

Utakatifu binafsi ni sharti msingi kwa Askofu


Katibu Kardinali wa Jimbo la Papa, Kardinali Pietro Palorin, Jumatano 10 Septemba, aliongoza Ibada ya Misa kwa ajili ya Maaskofu wapya walioteuliwa hivi karibuni , ambao wanashiriki katika kozi iliyoandaliwa na Decania ya Vatican kwa ajili ya Usharika wa Maaskofu na Baraza la Kipapa kwa Uinjilishaji wa Watu.

Kardinali Palorin katika homilia yake, aliwakumbusha Maaskofu kwamba, kuungana pamoja na Kristo ni maamuzi huru binafsi katika uaminifu wa kuishuhudia Injili na ufanisi wa utakatifu katika matendo ya kawaida. Kwa kuwa utakatifu wa Neno la Mungu hubaki kama ilivyo, zamani, hata sasa na siku zote za maisha ya mtu, Ukweli huu wa Neno la Mungu, unatahadharisha uangalifu wa kujua jinsi ya kusahihisha mafundisho, kazi za kichungaji na kiliturujia, pale inapoonekana hitaji la kufanya hivyo kwa Mafundisho ya Kanisa. Ni kuwa na utaratibu wa kusahihisha kinachokusudiwa kwa njia ya upendo, bila kuathiri imani sahihi ya waumini, na katika kuwa daima Mababa wanaoiga upendo wa Baba na Makuhani aminifu wahenga.

Kardinali pia aliyaelekeza mawazo ya Maaskofu wapya, kuwaombea waliofariki hivi karibuni kwa mateso na kuugulia, kwa sababu ya uaminifu wao kwa Kristo Bwana na upendo wao kwa ajili ya Kanisa.

Semina hii ya wiki mbili ya Maaskofu wapya, pamoja na Maaskofu kupigwa msasa, pia ni fursa ya kawaida inayokusudiwa Maaskofu wapya kukutana na kufahamiana. Kama ilivyokuwa siku ya Jumatano 10 Septemba katika Makao Makuu ya Chuo Kikuu cha Regina Apostolorum, Maaskofu wapya waliiitumia siku nzima, iliyoanza na Ibada ya Misa, iliyoongozwa na Kardinali Parolin na kuendelea na ripoti ya Kardinali Peter Turkson Kodwo, juu ya mafundisho ya kijamii ya Kanisa. Na AskofuMkuu Angelo Amato, alizungumzia juu ya maisha ya kiroho ya Askofu, na Askofu Mkuu Lorenzo Baldisseri juu ya Sinodi ya Maaskofu na umoja wa Maaskofu.

Semina hii ni utangulizi wa tukio la Hija ya Assisi, watakayofanya Maaskofu hao Jumapili 14 Septemba. Jumatatu, Maaskofu wataendelea na ratiba ya kozi kama ilivyopangwa.
All the contents on this site are copyrighted ©.