2014-09-13 11:26:40

Papa Francisco aalikwa kutembelea Istanbul wakati wa Sikukuu ya Mtakatifu Andrea


(Vatican Radio) Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, ametoa mwaliko rasmi kwa Papa Francisko kutembelea Uturuki. Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Ijumaa, Mkuu wa Ofisi ya habari Vatican Padre Federico Lombardi, alisema, Jimbo Takatifu limepokea mwaliko huo na liko katika maandalizi kwa ajili ya ziara ya Papa kwa Uturuki mwishoni mwa Novemba 2014. Hata hivyo bado haijajulikana ziara hii itakuwa ya siku ngapi, wala ratiba itakavyokuwa.

Papa anatarajiwa atembelee Istanbul, Mji Mkuu wa Uturuki hapo Novemba 30, ambayo ni Siku Kuu ya Mtakatifu Andrea, Mwanzilishi wa Kanisa la Mashariki na Msimamizi wa ulimwengu wa Waotodosi . Kila mwaka katika sherehe hizi, Makao Makuu ya Kanisa Ulimwengu, hutuma mjumbe wake kutoka Baraza la Kipapa kwa ajili ya Umoja wa Wakristo. Kwa mwaka huu Patriaki Bartholomayo 1 wa Upatriaki wa Kiekukemni wa Mashariki ya kati, siku za nyuma, amewahi kutoa mwaliko kwa Papa Francisko, ahudhuria sherehe hiz za Sikukuu ya Makatifu Andrea Uturuki mwaka huu. Papa Francisko, atakuwa anafuata nyayo za mtagulizi wake Mstaafu Papa Benedict XVI, ambaye alitembelea miji ya Ankara, Efeso na Istanbul Uturuki Novemba 2006.

Papa kuongoza mkesha wa sala kwa ajili Sinodi maalum ya Maaskofu
Vatican Radio) Taarifa imetolewa kwamba, Baba Mtakatifu Francisco, ataongoza Ibada ya maombi na sala ya mkesha, katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican, Jumamosi ya tarehe 4 Oktoba, kama ishara ya ufunguzi wa Sinodi Maalum ya Maaskofu , inayoongozwa na Mada mbiu "changamoto za Kichungaji kwa familia katika mazingira ya Uinjilishaji". Sala ya mkesha inaandaliwa na Maaskofu Katoliki wa Italia, kuonyesha pia umuhimu uliowekwa na Kanisa, juu ya jukumu la familia katika jamii ya leo. Mkesha wa maombi imepangwa kuanza saa 12 za jioni. Wakazi wa Roma , mahujaji na wageni nyote mwakaribishwa.

Mkutano wa Sinodi Maalum ya Maaskofu itakayo hudhuriwa na wajumbe 253, inaanza tarehe 5 -19 mjini Vatican na wajumbe wake wanatoka pande zote za dunia kwa lengo la kushirikisha mawazo na uzoefu katika maisha ya familia katika nyakati hizi, ambazo familia inakabiliwa na changamoto nyingi.All the contents on this site are copyrighted ©.