2014-09-13 09:22:56

Ahadi ya kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia na VietnamPapa Franciscko anafuatilia kwa karibu maendeleo katika mahusiano kati ya Jimbo Takatifu na Nchi ya Vietnam na uhamasishaji wa Wakatoliki katika kuchangia maendeleo ya nchi kwa manufaa ya wote na asasi za kiraia. Hilo lilielezwa Alhamis, baada ya kukamilika kwa Kikao cha 5 cha Tume ya pamoja ya wajumbe kutoka Viet Nam – Jimbo Takatifu. Kikao kilichofanyika mjini Hanoi Vietnam.


Taarifa inasema, kikao hiki cha siku mbili mjini Hanoi, tarehe 10 na 11 Septemba 2014, kilifanyika kwa utulivu , maelewano na urafiki, kama ambavyo ilvyokuwa katika vikae vyake vya awali,kikao cha mwisho kikiwa Vatican Juni 2013 , chini ya mwenyekiti mwenza, Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Vietnam, Mheshimiwa Bui Thanh aliyeongoza Ujumbe wa Vietnam, na Naibu Katibu wa Idara ya Vatican kwa ajili ya mahusiano na nchi za kigeni, Askofu Antoine Camilleri, kama mjumbe mwakilishi wa Jimbo la Papa.


Taarifa tokea kikao cha majuzi inaeleza kwamba, Ujumbe wa Jimbo la Papa, ulionyesha kupendezwa na msaada unaotolewa katika ngazi zote na Kanisa Katoliki nchini Vietnam katika utekelezaji utume wake. Na pia uliweza kuona maendeleo yanayofanyika katika sera ya kidini Vietnam kama ilivyo jitokeza mwaka 2013, haja ya kufanya marekebisho katika Katiba ya Vietnam, ili kwenda na nyakti za utandawazi. Na hivyo marekebisho hayo yamewezesha mjumbe wa Jimbo la Papa, Mons. Leopoldo Girelli kufanya ziara Vietnam. Ujumbe wa Jimbo la Papa umethibitisha hili na kutaja kuwa ni hatua muhimu katika kuendeleza mahusiano na Vietnam na Asia kwa ujumla, kama ilivyo jionyesha hivi karibuni wakati wa ziara ya Papa Asia.

Jimbo Takatifu, linalenga kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Vietnam na pamoja na Kanisa Katoliki katika nchi hiyo , kuwa na fursa ya kuchangia kikamilifu zaidi katika maendeleo ya nchi, hasa maeneo ya vijijini yanayoonekana kusahaulika ambako Kanisa Katoliki pia liko.
All the contents on this site are copyrighted ©.