2014-09-10 15:18:37

Mchango wa Jimbo Papa: Hakuna nafasi ya utumwa mambo leo.


Mwakilishi wa Kudumu wa Jimbo la Papa, katika Ofisi za Umoja wa Mataifa na mashirika yake yaliyoko mjini Geneva, Askofu Mkuu Silvano M. Tomasi, akizungumza katika Kikao 27 cha Baraza la Haki za Binadamu, juu ya utumwa mambo leo, alisisitiza, kupambana na utumwa mambio leo, dunia inahitaji kuhakikisha utu wa kila binadmau unalindwa, na watu wote kuwa na haki sawa , na kukataa kila aina ya ubaguzi na ukosefu wa haki unaoweza kumfanya mwingine, kutumikishwa kama mtumwa.

Askofu Mkuu Tomasi alieleza haya akirejea sababu na madhara ya kazi za kulazimishwa kama ilivyo ainishwa katika Ripoti ya Tume maalum, kwa ajili ya kutoa vipaumbele katika kipindi cha 2014-2017. Alionyesha kutambua tahadhari zinazotolewa na vyombo vya habari mbalimbali juu ya tatizo hili , akisema maelezo hayo yanapaswa kuivuta jumuiya ya kimataifa, kutazama ukweli wa tatizo hili kwa makini zaidi.

Katika mchango wake aliendelea kutoa angalisho katika taarifa za kutisha ikiwemo utekaji nyara na uuzaji wa watoto hasa wa kike kwa kisingizio cha mafundisho ya dini yanaruhusu kama wanavyo fanya Boko Haram huko Nigeria au kile kinachoendelea katika mkoa wa Kiislamu Kaskazini mwa Iraq. Takwimu zinaonyesha kundi la watoto zaidi ya 250,000, wameingizwa kwa nguvu kama "ngao ya binadamu" katika mstari wa mbele kwenye migogoro ya kivita.

Hivyo alisema , bila nia yoyote kupuuza au kupunguza wasiwasi wa muda mrefu juu ya aibu hii ya ukiukwaji wa hadhi ya binadamu, Jimbo Takatifu linaitambua Taarifa ya Mjumbe Maalum wa umoja wa Mataifa ambayo inapendekeza suala hili la utumwa mambo leo, lishughulikiwe kikamilifu, kwa kujali kwamba, kuna watoto zaidi ya milioni 5.7 waathirika wa kazi za kulazimishwa, zikiwemo ndoa za mapema, au za kulazimishwa, ndoa za kwa ajili ya kutumilikishwa na aina nyingine yoyote ile ya kazi isiyoheshimu utu wa mtu, zenye kuathiri maisha ya wengi, matatizo ambayo yako si tu katika nchi maskini lakini hata nchi tajiri.

Askofu Mkuu Tomasi anaendelea kusema, pamoja na kukubaliana na utengenezaji wa mianya mipya ya ajira hasa kwa vijana, kwa bahati mbaya, mbinu hizi zinafanyika zaidi kwa lengo la kutafuta faida zenye na hivyo hutengeneza mazingira yanayo hamasisha na kuwavutia watoto na vijana kuingia katika mtego huu wa kazi ya kulazimishwa na aina nyingine ya kisasa ya utumwakama ilivyobainishwa katika Ripoti ya Mwandishi Maalum. Na inaonyesha jinsi kunavyojitokeza shinikizo, katika mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na matukio ya ufukara, ukubwa wa wa familia na mgogoro wa kiuchumi, ukosefu wa elimu na kutojua kusoma na kuandika, ukosefu wa najira ya muda mrefu nana mambo mengine ambayo hulazimisha watu kuingia katika sekta hii isiyo rasmi, wakati mwingine ni kazi bila malipo, na uhamiaji wa bila hiari, na biashara ya binadamu.

Jimbo la Papa pia limeonyesha kutambua juhudi zilizopo za Jumuiya ya kimataifa, kwamba ni kweli tayari inajaribu kutekeleza,mikataba mbalimbali ya kimataifa na mikataba ya kulinda dhidi ya aina ya utumwa wa kisasa. Hata hivyo Jimbo la Papa lina amini, vyombo hivyo haviwezi kukidhi malengo kikamilifu, kama hapatakuwa na ufuatiliaji wa karibu wa mara kwa mara na utashi mpana wa kisiasa na ushiriki wanachama wote wa jamii ya kimatifa.

Jimbo la Papa linaona , tunahitaji kuvunja ukimya juu ya jambo hili la aibu katika dunia iliyostaraabika. Utumwa mambo leo ni jeraha wazi juu ya mwili wa jamii ya kisasa. Jeraha lenye kuhamasisha wanaume na wanawake wenye mapenzi mema, kupiga ukelele wa sasa basi yatosha, kama anavyofanya Papa Francisco mara kwa mara, ndivyo inavyotakiwa kwa wote kukemea madhulumu haya. Kazi za Kulazimisha ni kuchukizo kwa wengi, na utumwa huo, unaendelea katika dunia ya leo.

Jimbo la Papa linaunganana na viongozi kutoka mila nyingine na dini zote zenye kukuza maadili ya amani na maadili ya pamoja na ubinadamu ili kuondoa utumwa wa kisasa na biashara yake haramu ya binadamu katika dunia yetu kwa wakati huu na wakati ujao. . Baba Mtakatifu Francisco, katika kukerwa na jambo hili, ametangaza mandhari, ya adhimisho la 40 la Siku ya Amani duniani hapo Januari Mosi kuwa:"Hakuna tena utumwa, lakini sisi sote ni ndugu, kaka na dada.








All the contents on this site are copyrighted ©.