Jumatatu 8Sept 2014 nchini Iraq, baraza jipya la mawaziri limetangazwa, hata hivyo
hakuna Waziri wa ulinzi wala wa mambo ya ndani ya nchi aliyetangazwa mpaka sasa. Lakini
waziri mkuu wa nchi hiyo amesema atafanya uteuzi wa mawaziri hao kwa muda wa wiki
moja. Naye Waziri wa mambo ya nje wa marekani john Kerry amelikaribisha baraza
jipya la mawaziri lililotangazwa nchini Iraq, na kusema kuwa baraza hilo litaleta
manufaa ya taifa hilo. Akisisitizia msimamo wa Marekani, alisema kwamba serikali
yake itashirikiana kwa karibu na serikali hiyo. Waziri Mkuu Haidar al Abadi, amewaambia
waandishi wa habari kuwa huenda serikali hiyo ikasababisha nchi yake kuondokana na
makundi ya wapiganaji wanaotishia usalama wa taifa hilo, endapo kutakuwa na kuaminiana
miongoni mwa wananchi. Nafasi nyingine za mawaziri zimejazwa kwa mujibu wa makubaliano
kati ya Washia walio wengi, Wasunni hali kadhalika na Wakurd walio wachache. Wakati
hayo yakijri watu 12 wameuawa na wengine zaidi ya thelathini wamejeruhiwa jumatatu
wiki hii katika shambulio la bomu liliyotegwa ndani ya gari dhidi ya msafara wa kikosi
cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika AMISOM kaskazini mwa mji mkuu wa Somalia, Mogadiscio,
viongozi wa somalia wamethibitisha. Abdulkadir Sidi, mkuu wa mkoa wa Shabelle ya
Chini amabako shambuli hilo lilitiokea alisema kuwa “ Gari iliyojazwa vilipuzi ilisukumwa
ikielekezwa kwenye kifaru cha Kikosi cha wanajeshi wa AMISOM na raia 12 wa kawaida
waliokua wakisafiri ndani ya basi wameuawa na wengine 27 wamejeruhiwa na, Wanajeshi
wawili wa AMISOM wamejeruhiwa pia katika shambulio hilo.
Wasiwasi wa
vita umetanda Ukraina Bado mashambulizi mapya yanaendelea kutokea mwanzo
mwa wiki hii karibu na mji wa mwambao wa Marioupol, mwashariki wa Ukraine,miliyo ya
risasi na mizito naendelea na kupelekea makubaliano yakusitisha mapigano kuwa hatarini.
Kundi moja la raia wa Ukraine waliyojitoa muhanga kwa kupigania uhuru wa Ukraine wameshambuliwa
kwa bomu jumapili mwishoni mwa juma liliyopita kwenye moja ya ngome yao katika mji
wa Marioupol, huku milipuko ya mabomu ikiendelea kusikika usiku mzima wa jumapili.
Hali
ya wasiwasi imeendelea kutanda nchini Ukraine, licha ya viongozi wa Urusi na Ukraine
kusaini makubaliano ya kusitisha mapigano mashariki mwa Ukraine.
Wakati wa
mazungumzo ya simu pamoja na kansela wa Ujerumani, Angela Markel, rais wa Ukraine
Petro Porochenko amejizuia kusema kinachoendelea mashariki mwa Ukraine, huku akiendelea
kupongeza juhudi za kusaini makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Urusi na Ukraine
mjini Minsk.
Rais porochenko amekuwa na imani ya kutuma tume ya waangalizi
wa jumuiya ya usalama na maendeleo barani Ulaya kwenye eneo kunakoshuhudiwa mapigano,
huku akiwa na imani kwamba masharti ya kusitisha mapigano yatakua yametekelezwa kabla
ya kuunza kwa mazungumzo kati ya pande zinazo husika katika machafuko hayo.
Viongozi
wa waasi wa Ukraine wamependekeza kuongezwa kwa ibara ya kuutambua uhuru wa maeneo
yanayothibitiwa na waasi kwenye makubailiano ya kusitisha mapigano yaliyosainiwa mjini
Minsk.
Misri : Ushirikiano wa nchi za Kiarabu wakubaliana kushirikikiana
kupambana na wababe wa jihad Mawaziri wa mambo ya nje wa jumuiya ya nchi
za kiarabu, jumapili Septemba 7 mwaka 2014 mjini Cairo, nchini Misri walikubaliana
kuchukua hatua zinazohitajilka kukabiliana na waislamu wababe wanaozusha vita vya
jihad, pamoja na kutoa ushirikiano wao katika juhudi za kimataifa, kikanda au kitaifa
kwa kupambana na makundi ya kiislam yenye silaha. Katika kikao hicho mawaziri hao
wamekubaliana kusitisha misaada ya kijeshi hususani silaha na vifaa vingine vya jeshi
pamoja na fedha kwa makundi ya kiislam yenye silaha nchini Iraq na Syria. Azimio
la jumuiya ya nchi za kiarabu ni kujilinda kwa mataifa wanachama wa jumuiya hiyo dhidi
ya vitisho vya Dola la Kiislamu pamoja na makundi mengine ya kiislam ya kigaidi katika
ulimwengu wa kiarabu. Katibu wa jumuiya ya nchi za kiarabu, Nabil Al Arabi alisema
“ Hatutokubali kuendelea kwa vitisho hivyo ya Dola la Kiislamu”, . Kuongezeka kwa
makundi ya wapiganaji wa kiislamu wenye msimamo mkali imekuwa ni tishio kwa mataifa
wanachama wa jumuiya ya nchi za kiarabu, hadi kupelekea baadhi ya mataifa hayo kuvunja
ushirikiano wao na makundi hayo. Azimio la jumuiya ya nchi za kiarabu linatoa fursa
kwa taifa lolote mwanachama wa jumuiya hiyo kutoa ushiriki wake kwa Marekani ambayo
imekua ikitoa wito kwa mataifa kushirikiana kwa pamoja dhidi ya Dola la Kiislam. Kenya:
Magazvana watakiwa kuunga mkono wito wa kujiuzulu Rais Uhuru Kenyatta
amewataka magavana wa Muungano wa Jubilee wanaounga mkono wito wa Cord wa kuandaa
kura ya maamuzi kujiuzulu mara moja na kuwania upya nyadhifa zao. RAIS Uhuru Kenyatta
amewataka magavana wa Muungano wa Jubilee wanaounga mkono wito wa Cord wa kuandaa
kura ya maamuzi kujiuzulu mara moja na kuwania upya nyadhifa zao. Alisema magavana
hao wanakwenda kinyume na sera ya muungano tawala kuhusu ajenda ya maendeleo. Akizungumza
jumapili 7Sept katika Kaunti ya Kericho alipohudhuria ibada katika Immanuel Africa
Gospel Church (AGC), alisema viongozi wa Jubilee ni sharti waungane kupinga shinikizo
la kuandaa kura ya maamuzi. Huku akihutubia umati wa watu mjini Kericho baada ya
kutoka kanisani, Rais Kenyatta alisema hakuna mgawanyiko baina ya chama chake cha
The National Alliance Party (TNA) na kile cha Naibu Rais William Ruto, United Republican
party (URP). Aliwalaumu magavana waasi wakiongozwa na mwenyekiti wa Baraza la Magavana
na kiongozi wa Kaunti ya Bomet Isaac Ruto kuwa wanasaliti muungano tawala wa Jubilee.Aidha
aliwataka magavana waasi kuwaambia Wakenya ukweli kuwa watatozwa ushuru zaidi endapo
kiasi cha fedha zinazotolewa kwa serikali za kaunti kitaongezwa. Alisema kuwa serikali
haina fedha zaidi za kupatia serikali za kaunti. Alishangaa kwa nini wakuu hao
wa kaunti wamekuwa wakitaka waongezewe fedha zaidi, hali wameshindwa kueleza namna
walitumia fedha walizopokea kwenye kipindi cha fedha cha mwaka uliopita. Rais alitetea
serikali yake dhidi ya madai kuwa inajaribu kudhoofisha ugatuzi, huku akisema kuwa
Jubilee imekuwa ikifanya kila iwezalo kuhakikisha kuwa inatekeleza katiba mwaka mmoja
tangu kutwaa hatamu za uongozi. Tanzania:onyo kwa vyama vinavyo vyenye uchochezi
Katika Kamati za Bunge linaloendelea nchini Tanzania ,baadhi ya taarifa
na mapendekezo ya tume mbalimbali zinazidi kuchangamsha Bunge hilo, kwani baadhi ya
Kamati za Bunge Maalumu la Katiba zimependekeza kuwekwa kwa masharti ya kudhibiti
vyama vya siasa ambavyo vitaendesha siasa za uchochezi na ubaguzi wa dini, jinsia
au kuegemea eneo fulani tu katika upande wowote wa Jamhuri ya Muungano kufutiwa usajili
wake. Pendekezo hilo lilitolewa kwa nyakati tofauti na Kamati Namba nane na Namba
kumi wakati zikiwasilisha taarifa za mijadala yake, bungeni mjini Dodoma Ijumaa 5Sept
ya wiki iliyopita. Kamati Namba nane ilipendekeza kuandikwa upya ibara ya 197 (2)(a-d)
ya Rasimu ya Katiba kwa kuongeza masharti hayo. Akisoma mapendekezo hayo, mjumbe
wa kamati hiyo, Lucas Malunde alisema kamati hiyo inapendekeza kufutwa kwa chama ambacho
kinakubali au kupigania matumizi ya nguvu au uchochezi kama njia za kufikia malengo
yake ya kisiasa. Alisema sharti hilo litahusika kama ikibainika chama cha siasa
kitaonekana kupigania au kukusudia kuendesha shughuli za kisiasa katika upande mmoja
wa Jamhuri ya Muungano. “Katika ibara 197 (4) kamati imependekeza Bunge linaweza
kutunga sheria inayoweka masharti sawa yatakayohakikisha vyama vya siasa kuzingatia
mipaka na vigezo na masharti ya ibara hiyo,” alisema.