2014-09-10 15:26:15

Idadi ya washiriki katika sinodi maalum ya Maaskofu yatajwa


Katibu Mkuu wa Sekretariati ya Sinodi Maalum kwa ajili ya Familia ya Oktoba 2014 hapa Vatican, Askofu Mkuu Bruno Forte , wa Jimbo Kuu la Chieti- Vasco, katika mahojiano na Redio Vatican, ametaja idadi ya washiriki wa sinodi hiyo kuwa 253 . Miongoni mwao kutakuwa na jozi 14 za wanandoa.

Askofu Mkuu Bruno, amefafanua neno “Sinodi” kwamba maana yake ni "kutembea pamoja. Na hivyo wakati wa mkutano huo wa Sinodi, watu kutoka bara tano za Kanisa zima la ulimwengu, watatembea pamoja wakikiekea Kiti cha Petro, kwa ajili ya kutafakari pamoja, “changamoto za Kichungaji katika mazingira ya uinjilishaji. Na kwamba wingi wa washiriki 253 katika Sinodi hii,unaweka rekodi nyingi katika historia ya Sinodi za Vatican, baada ya ile ya 1969 na 1985, katika mtiririko huo, unaohusiana na mikutano ya Maaskofu katika ushirikiano wao na matumizi ya Mtaguso Mkuu wa II.

Na kwamba, Mababa wa Sinodi watakuwa 191, ikiwa ni pamoja na wakuu wa idara ya 25 Curia na 114 Marais wa Mabaraza ya Maaskofu: 36 kutoka Afrika, 24 kutoka Marekani, 18 kutoka Asia (China, kutakuwa na Askofu Mkuu wa Taipei, Msgr. Shan-chuan), 32 kutoka Ulaya, ikiwa ni pamoja na Kardinali Angelo Bagnasco Italia, na 4 kutoka Oceania.

Aidha kutakuwa na washiriki wengine 62, ikiwa ni pamoja na 8 kutoka ushariki wa kidugu na kanisa la Kiotodosi, akiwemo Patriaki Hilarion, Mwenyekiti wa Idara ya Uhusiano wa Nje wa Upatriaki wa Moscow..Na kutoka Makanisa ya Mashariki kutakuwa na wajumbe 13, pia kutoka nchi zenye vita, kama vile Iraq na Ukraine, wakiwakilishwa na Askofu Mkuu Louis Sako na kutoka Makanisa Katoliki ya Kigiriki-Katoliki Shevchuk. Aidha 13 watakuwa wanandoa ambayo watakuwa sehemu ya wasikilizaji 38, wenye haki ya kuongea lakini si kupigia kura maamuzi ya Sinodi; kuna Washauri wawili na pia kuna kundi la watalaam 16 , watakao fanya kazi za kusaidia Sekretariati ya Sinodi Maalum. Miongoni mwa wajumbe walioteuliwa na Papa, ni Padre Antonio Spadaro, Mkurugenzi wa gazeti Jesuit "Civilta Catoliki".

Wakati wa wiki mbili za kazi, washiriki wa Sinodi, watatafakari juu ya matokeo ya rasimu ya kufanyia kazi iliyosambazwa mwezi Juni. Lengo, anasema Kardinari Lorenzo Baldisseri, Katibu Mkuu wa Sinodi, ni kwa "kutoa pendekezo katika dunia ya leo uzuti na tunu za madili ya familia , kama ilivyotangazwa na Yesu Kristo zenye kufuta hofu zote na kuinua matumaini endelevu."

Kama ambavyo ilikwisha tangazwa awali katika Mkutano wa Kawaida wa Sinodi ya Maaskofu, kazi za Sinodi hii maalum kwa ajili ya Familia, zitafuata mbinu mpya, katika upendeleo wa kuwa na washiriki wengi zaidi wa Mababa wa Sinodi. Anaelezea kadi. Baldisseri, "kufanya marekebisho ya sheria au pengine kuweka kuwa na marekebisho halisi katika baadhi ya vipengere", Na kwamba hawatarajii kuwa na waraka wa mwisho mwishoni wa Sinodi hii maalum, kwa kuwa hii ni tu hatua ya kwanza ya safari, itakayokamilika mwaka 2015, Oktoba 04-25, wakati wa Mkutano 14 wa Sinodi ya kawaida juu ya mada "Yesu Kristo ataonyesha siri na wito wa familia.
All the contents on this site are copyrighted ©.