2014-09-09 07:50:40

WFP-yazindua michezo ya raga


Hivi karibu ShirIka la mpango wa Chakula , ( WFP) na Bodi ya Kimataifa ya Michezo ya Raga ulizindua mpango maalumu ya ukusanyaji wa fedha na kukuza uelewa kama sehemu ya kupambana na njaa wakati wa kombe la dunia la michezo ambao utafanyika Uingiereza mwaka 2015.
Lengo la mpango huo ni kuhakikisha kwamba kabla ya kufanyika kwa michuano kufikia mshindi wa tatu maarufu kwa ukubwa ulimwenguni ambayo itaanza September 18 mwakani kesho, kuwepo kwa juhudi za kuchangisha fedha katika mradi uitwao Million Meal Challenge ya kuwasaidia wanafunzi walioko nchi zinazoendelea kupata chakula.
Ushirikiano wa Kombe la Dunia la Raga ya Kupamba na njaa umefanikiwa katika kuongeza uelewa sawa na kusaidia kazi ya shirika la mpango wa chakula (WFP) katika kuwalisha watu walio na njaa duniani.
Michuano hiyo itakayofanyika nchini Uingereza inakisiwa kuwa mikubwa zaidi kuwahi kufanyika, na mashabiki wanazidi kuchangia katika Million Meal Challenge.
Kufikia sasa zaidi ya Dola $ 21,000 zimechangishwa kama kupitia katika mchango wa hiari, kupitia mauzo ya tiketi, kupitia mtandao nchini Uingerea, huku mauzo ya tiketi kwa mashabiki wa kimataifa yakizinduliwa September 12.

MKUTANO WA WADAU KATIKA SEKTA YA MIFUGO MWANZA -TANZANIA
Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, ulifanya mkutano mkoani Mwanza nchini Tanzania wa siku tatu wiki iyopita kwa ajili ya sekta ya mifugo kwa mikoa yenye mifugo mingi na kuwashirikisha wakuu wa mikoa , wilaya na makatibu tawala.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika ufunguzi wa mkutano huo aliwataka wafugaji nchini kufuga kisasa ili kuwavutia wawekezaji kibihashara na kuongeza kipato kwaajili ya kuondokana na umasikini..
Akivutia umuhimu wa mifugo alisema "Nyie wadau zaidi ya 400 wa mifugo mliopo hapa, jaribu kubadilika katika suala la ufugaji, fugeni kisasa ili muone ndege kutoka Ulaya zinafuata minofu ya nyama kama zilivyokuwa zikifuata minofu ya samaki,"
Waziri Mkuu alisema endapo wafugaji watajitambua, kufanya ufugaji wa kibiashara anaamini sekta ya mifugo itakuwa na mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa taifa.
Aidha alishangazwa na kitendo cha mkulima anayelima mazao kwa shida kuishi bora kuliko mfugaji anayepata mifugo mingi bila kutumia mtaji mkubwa.
Waziri Pinda alizungumzia njia mbalimbali za kukabiliana na changamoto zinazojitokeza kwa wafugaji ikiwa ni pamoja na kupunguza migogoro ya ardhi isiyokuwa ya lazima, kuimarisha miundombinu katika ufugaji ikiwa ni pamoja na kuboresha malambo, malisho ili kuifanya mifugo isitange tange kutafuta sehemu ya malisho. Pia aliwataka watendaji mbalimbali kujitoa nje na kufanya kazi kwa kuanzia ngazi ya chini, kati hadi juu ili kujua matatizo ya wafugaji hatua aliyosema kwa sasa iko katika hali nzuri.
Kuhusu changamoto zinazokabili sekta hii ya ufugaji Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Titus Kamani alisema wafugaji wa asili wanachangamoto nyingi ambazo kunatakiwa nguvu ya pamoja katika kuzikabili, na changamoto hizo ni pamoja zana duni za malisho ambapo tatizo hilo linaendelea kuongezeka hasa kwa wakati wa kiangazi ambapo malisho hupungua kwa kiasi kikubwa.
Hata hivyo, alisema serikali inaokoa zaidi ya Sh.trilioni 20 kutokana na kutumia chakula kinachotokana na mifugo na kwamba ingekuwa kuagiza nje ingekuwa na ugumu.
Aliongeza jumla ya kaya 1,745 zinajishughulisha na mifugo ambazo ni sawa na asilima 35 ya kaya 4,901 zinazojishughulisha na kilimo na mifugo.
Kuhusiana na migogoro ya ardhi Waziri wa Ardhi Prof. Anna Tibaijuka alisema kuwa matatizo mengi ya ardhi yanatokana na kuhamishwa kwa mifugo inayosababisha migogoro mikubwa kati ya wakulima na wafugaji.

EBOLA KUJADILIWA NA WATAALAMU 200 USWIZI
Takribani wataalamu 200 wa Ebola wamekutana huko Uswizi kuzungumzia uwezekano wa tiba na chanjo kwa ugonjwa huo, huku idadi ya kesi ikiendelea kuongezeka katika mataifa ya Afrika magharibi.
Shirika la afya duniani-WHO linasema mkutano huo wa siku mbili huko Geneva ilikuwa ni wa kutathmini maendeleo ya karibuni juu ya uwezekano wa matibabu kwa Ebola na kutaja hatua muhimu sana ambazo zinahitajika kuchukuliwa.
Hakuna matibabu au chanjo kwa ugonjwa huu unaosababisha kifo, japokuwa dawa ya majaribio ya Zmapp, iliyotengenezwa na kampuni moja ya Marekani imetolewa kwa idadi ndogo ya wagonjwa, baadhi ya wagonjwa hao wamepona.
Mkurugenzi mkuu wa WHO, Margaret Chan alisema jumatano iliyopita kwamba mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika mataifa ya Afrika magharibi hivi sasa umeuwa zaidi ya watu 1,900 na umewaambukiza watu wasiopungua 3,500, wengi katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone.

Wakati huo huoi Nchi ya Sierra Leone ambayo inaongoza kwa ugonjwa huo na Pia Liberia imetoa tamko kwamba italazimaka watu wake kubaki nyumbani kwa siku nne kuanzia tarehe 18-21Sept kwaajili ya kugaguliwa na chombo maalumu, kwaajili ya kuzuia maambukizi ya virusi hivyo.
Ni uamuzi ulitolewa na wahudumu wa afya kwaajili ya kuchunguza na kuwatambua wale ambao wana ugonjwa huo , wasiendelee kusambaza zaidi.
Hayo yalielezwa na Bwa Ibrahimu Ben Kargbo ,mwenyekiti mshauri wa madaktari ya wasio na mipaka nchini Sierra leone.
Bwana alisema hili kupambana na virusi hivyo ni lazima kukabiliana na jambo hili mara moja; Japo itakuwa ni kazi ngumu kwa wahudumu wa wafya kubaihinisha watu wenye maambukizi hayo kwa kutumia chombo cha ukaguzi wakibisha hodi nyumba kwanyumba.
Pamoja na hayo alisema kwamba nchini Sierra leon, kunu uhaba mkubwa wa nafas iza wagonjwa mahosptalini.
Ni Zaidi ya wahudumu wa afya 21,000 watakaozungukia nyumba kwa nyumba, kwa kufuatia hata maelelezo na makubaliano ya mkutano Mkuu wa Afya duniani wa wataaalumu 200 walikutana huko uswizi.
All the contents on this site are copyrighted ©.