2014-09-09 08:18:13

Papa - vita havina maana


Ujumbe wa Papa kwa Mkutano wa Dunia wa Viongozi wa Kidini, unasema vita haina maana kwa kuwa haiwezi kurekebisha tatizo la ukosefu wa haki. Haki hupatikana katika kuheshimiana, mazungumzo na ushirikiano, hizo ndizo silaha zinazofaa kudumisha haki na maridhiano.

Ni maneno ya mazito yaliyomo katika ujumbe Papa, kwa mkutano wa kila mwaka unao andaliwa na Jumuiya ya Sant'Egidio. Mkutano huo kwa mwaka huu, unafanyika chini ya Madambiu"Amani ni siku zijazo. Ujumbe wa Papa Francisko ulisomwa kwa washiriki wa Mkutan, siku ya Jumapili mchana , wakati wa sherehe za ufunguzi wa mkutano huo, unao fanyika mjini Antwerp, Ubelgiji. Mkutano unakamilika Jumanne hii.

Francesca Sabatinelli, wa Redio Vatican, ametaarifa tokea mkutano, na kwamba, Papa umetaja mizozo yenye kusababisha umwangaji wa damu, inayoshuhudiwa siku hizi, unawarejesha washiriki kutafakari kwa kina somo lililotolewa kwa dunia, kutoka Vita vya dunia ambavyo vimetimza miaka miaka mia, tangu kuzushwa.

Maadhimisho haya - anasema Papa Francisko, yanatoa somo kwamba, vita kamwe si njia inayofaa kuondoa madhulumu na kutotendewa haki. Ni tu katika njia ya mashaurianao na maridhiano, huweza kumaliza ugomvi wa kisiasa na kijamii kwa amani. Kila vita, aliongeza kwa kumnukuu Benedict XV katika waraka wake wa mwaka 1917, huwa ni umwangaji wa damu usiokuwa na maana. Vita huwaweka watu katika mduara wa hali ngumu na vurugu ambazo udhibiti wake unakuwa mgumu , na hivyo kuvuruga mema na maendeleo yote yaliyokwisha jengwa na wahenga. Vita ni njia ya udhalimu yenye kujenga migogoro zaidi.

Papa alieleza bila ya kutaja eneo lolote lenye kuwa na migogoro na vita kwa wakati hii, lakini alisema vita vinavyoendelea leo hii vinachoma mioyo ya watu, na vina angamiza maisha ya vijana na wazee. Vita ni sumu ya mshikamano wa makundi ya kikabila na kidini, vyenye kulazimisha jamii nzima kuishi uhamishoni, ambako wanapambana na mateso bila ya huruma, wengi wakipoteza maisha. Hapa ndipo, tunaona maana ya hatua hii ya kuunganisha viongozi wa dini mbalimbali, kujumuika pamoja katika Roho wa Assisi, kwa nia ya kutoa mchango kwa amani duniani, kupitia njia ya maombi ya pamoja na mazungumzo.

Papa amesisitiza vita -havina maana yoyote, na vinaweza kuepushwa. Daima inawezekana kupata mbadala kupitia njia ya mazungumzo na tafiti za dhati na kweli katika kupata jawabu linalofaa wote.

Kwa hiyo Francesko, amewaomba viongozi wa dini walio kusanyika Ubelgiji, kufanya kazi kwa ushirikiano wa dhati kwa ajili ya ufanisi katika matendo ya kuponya majeraha, kutatua migogoro inayokera wanaume na wanawake, kwa njia ya amani. Jumuiya zetu, ujumbe unahitimisha, ni “shule” ya heshima na mahali pa mazungumzo na wote, kikabila au kidini na makundi mengine. Ni eneo ambapo tunajifunza kushinda mvutano, na kukuza mahusiano ya usawa na amani kati ya watu na makundi ya kijamii na kujenga dunia iliyo bora ya baadaye kwa vizazi vijavyo. Na huo ndiyo ujumbe msingi wa mkutano huu ulioandaliwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio kila mwaka.
All the contents on this site are copyrighted ©.