2014-09-08 16:45:00

Maaskofu wa Cape Verde kuanza hija yakitume Vatican Jumatatu.


Maaskofu Katoliki katika Nchi ya Visiwa vya Cape Verde, wanatazamia kuanza ziara yao ya kitume hapa vatican ambayo hufanywa na Maaskofu kwa kawaida kila baada yamiaka mitano, kuyatembelea Makao Makuu ya Kanisa na kukutana na Papa, kwa lengo la kutoa taarifa na uzoefu wa kanisa katika kipindi hicho cha miaka mitano na matazamio ya utendaji katika kipindi kinachofuatia, ikiwa pamoja na ushirikiano na mshakamano kati ya Maaskofu na Papa katika kuliendeleza Kanisa la Kristo.
Kanisa Katoliki katika viiswa vya Cape Verde, halina Baraza lake la Maaskofu, na majimbo yake mawili yaliyoundwa moja kunako mwaka 1533 Jimbo la Santiago di Capo Verde, linaongozwa na Askofu Arlindo Gomes Furtado na Jimbo la Mindelo, liliundwa mwaka 2033 na linaongozwa na Askofu Ildo Dos Santos Lopes Fortes. Majimbo hayo yako chini ya Baraza la Maaskofu Katoliki linalounganisha Maaskofu wa Senegal, Mauritania, Capo verde na Guinea Bissau , na pia ni mwanachama katika Baraza la Maaskofu wanaozungumza Kifaransa Afrika Magharibi (CERAO), na SECAM.
Idadi kubwa ya raia wa Visiwa vya Cape Verde, ambavyo viko karibu na Pwani ya Senegal, wapatao milioni 1.5, ni Wakatoliki wanaofikia asimia 93 ya raia wote, kwa mujibu wa takwimu za Kanisa za Mwaka 2011. Na iliwahi kutembelewa na Baba Mtakatifu Yohane Paulo 11, terehe 25-27 Januari 1990, ambayo ilikuwa ni ziara yake ya kimataifa ya 45.










All the contents on this site are copyrighted ©.